YANGA YAIFUNGA RHINO 3-0
Wakicheza
kwa umakini, timu ya Yanga ya Dar es salaam imefanikiwa kuwafunga Rhino Rangers
ya Tabora kwa magoli 3-0, goli moja
likifungwa katika kipindi cha kwanza na
mawili kipindi cha pili katika mchezo ambao Yanga waliutawala kwa muda mwingi.
![]() |
| JUMA BADUL AKIMUACHA VICTOR HANGAYA WA RHINO |
Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa
aliwasumbua sana walinzi wa pembeni wa Rhino kwani hawakua na njia nzuri ya
kumzuia na kumfanya apige pasi na krosi nyingi kuelekea langoni mwa Rhino. Na Simon Msuva alianza mchezo huo vizuri na kwa
umakini mkubwa lakini kadri muda ulivyozidi kwenda alipoteza umakini na kufanya
maamuzi mengi ambayo hayakua na uhakika,na akawa anajiangusha ili apate faulo matokeo yake akapewa kadi ya
njano. Alikuja kutolewa katika dakika ya 59.
Yanga walibadili kikosi chao
tofauti na kilichozoeleka na ambacho kilicheza na Simba katika sare ya
3-3, walimuweka Juma Abdul kama beki wa
kulia badala ya Mbuyu Twite aliyecheza beki wa kati, na Zahir Rajab katika kiungo wa chini nafasi
ya Atumani Iddi na mbele akaingia Simon Msuva ambae alicheza pembeni na katikati akasimama Hamisi Kiiza na Mrisho
Ngasa,hivyo Athumani Iddi,Didier Kavumbagu na Nadir haroub hawakupangwa
kabisa,na golini alikuwepo Deogratius Munishi badala ya Ally Mustafa.
![]() |
| HAMISI KIIZA AKISHANGILIA GOLI |
Goli la kwanza la Yanga
lilipatikana baada ya Simon Msuva kupokea mpira toka kwa Zahir na akakimbia
pembeni akimuacha kirahisi beki wa kushoto wa Rhino Hussein Abdallah na kupiga
krosi iliyompita Ladislaus Mbogo na kumkuta Kiiza aliyeupeleka wavuni,ilikua ni
dakika ya 12. Waliendelea kutawala na kuwapoteza kabisa viungo wa Rhino
Stanslaus Mwakitosi,Imani Ndeli na Nurdin Bakari ambao muda mwingi walikua
wakiutafuta mpira bila mafanikio.
Yanga walifanikiwa kupata bao la
pili katika dakika ya 72 lililofungwa na kiungo wao Frank Domayo aliyemalizia
kazi nzuri ya Mrisho Ngasa aliyempita kwa umaridadi beki wa kushoto WA Rhino na
kutoa pasi nzuri kwa Domayo aliyemalizia kirahisi.Rhino hawku na mipango ya
kutafuta goli kwani hata golikipa wa Yanga Meogratius Munishi hakuokoa hata hatari moja,muda wote wa mchezo
alikua kama mtazamaji.
![]() |
| MBUYU TWITE AKIMDHIBITI IMANI NDELI |
Goli la tatu lilifungwa tena
na Hamisi Kiiza na kumfanya afkishe magoli saba katika ligi hii,lilipatikana
baada ya mpira ulioppigwa na Ngasa kumshinda Nurdin Bakari aliyeteleza na
kuanguka na mpira kumfikia Kiiza aliyeupeleka pembeni mwa goli la Rhino na
kuandika goli la tatu.Kwa ujumla Yanga walicheza vizuri sana katika mchezo huo
na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga tofauti na Rhino ambao walikua kama
hawajajitayarisha kwa ajili ya mchezo huo.
![]() |
| HAMISI KIIZA,DOMAYO,NIZAR NA NGASA |
VIKOSI;
YANGA-Deogratius Munishi,Juma Abdul,David
Luhende,Mbuyu Twite,Kelvin Yondani,Zahir Rajab,Simon Msuva,Frank Domayo,Hamisi
Kiiza,Mrisho Ngasa,na Haruna Niyonzima.
RHINO- Mahmoud Othman,Ally Mwanyiro,Hussein
Abdallah,Julius Masonga,Ladislaus Mbogo,Stanslaus Mwakitosi,Shija Mongo,Imani Ndeli,Victor
Hangaya,Saad Kipanga na Nurdin Bakari.




No comments:
Post a Comment