Alex seth
Messi wa
mbeya city
IMEANDIKWA NA ABDUL SUDI,PICHA KWA HISANI YA ALEX SETH
Anapiga miguu yote miwili, jambo ambalo
ni nadra sana kwa wachezaji wengi, ana
uwezo wa kufunga na pia ni mzuri sana wa
kupiga pasi za mwisho. Huyo ni Alex Seth
au maarufu sana kwa mashabiki wa soka kama Messi wa Mbeya City.
 |
| KABLA YA KUPAMBANA NA YANGA |
Ingawa ana umri mdogo wa miaka 19, lakini si muoga
kwa mabeki hata wale wanaosifika kwa kucheza faulo, anavyozidi kufanyiwa faulo,
inakua kama unampa hamu zaidi ya kutaka kupita kwa lazima, atakupiga chenga, atakutoka
kwa kasi na pia anatoa krosi nyingi zenye akili.
 |
| ALEX (WA PILI KUSTOKA KUSHOTO MBELE) AKIWA NA KIKOSI CHA CITY |
Alizaliwa mkoani Ruvuma na kupata elimu
yake hapo hapo Ruvuma katika shule ya sekondari Msamala, na alikua ni mchezaji
wa kutumainiwa wa timu ya shule,na hata katika timu ya Kambarage kids kisha
MajiMaji ikiwa daraja la kwanza.
 |
| WAKATI WA MCHEZO NA JKT OLJORO |
Alipomaliza kidato cha nne kocha Juma
Mwambusi aliamua kumchukua ili wasaidiane kuipandisha daraja timu ya Mbeya
City, jambo ambao walilitimiza na kufanikiwa kuingia katika ligi kuu.
Na hata timu ilipopanda amefanikiwa
kucheza mechi kadhaa, ikiwemo mechi ya
kwanza kwa Mbeya City kucheza ligi kuu ya Tanzani pale walipocheza na Kagera
Sugar. Toka hapo ameweza kucheza michezo kumi kati ya kumi na tatu timu yake
iliyocheza.
 |
| BAADA YA MECHI NA MGAMBO MKWAKWANI TANGA |
Akiizungumzia timu yake ya Mbeya City
anasema kikubwa kinachowafanya wafanikiwe hadi kufikia hatua hii ni jinsi
walivyo pamoja kwani mchezaji hata ambae hakucheza katika mchezo husika hua
anashiriki kwa asilimia mia moja kuhakikisha anawapa hamasa wale wanoacheza,
hakuna mazengwe kama wanayoyasikia kwa timu nyingine.
 |
| ALEX (WA KWANZA KUSHOTO)WAKATI WA MECHI NA SIMBA,UWANJA WA TAIFA |
Pia hakusita kuwasifia mashabiki wa timu
hiyo kwani kila wanapocheza wanakua kama wana kitu cha ziada nje kinachowasukuma wafanye vizuri . “tazama mchezo wetu na Azam, tulicheza ugenini lakini jinsi mashabiki wetu walivyokua wengi ilikua kama
tunacheza jijini Mbeya! Walikua ni zadi ya nusu ya uwanja, ukitazama wengi
walikua wamesafiri kuja kutupa sapoti, hilo nalo linaongeza nguvu na kutufanya
tupigane ili tusiwaangushe.”alisema.
 |
| MASHABIKI WA MBEYA CITY KABLA YA MECHI NA AZAM |
“Na kitu kingine kinachotufanya tuwe makini ni ubora wa kocha wetu Juma Mwambusi, kwani yupo karibu sana na sisi na habagui mchezaji,
kama anakuweka benchi anakuambia kabisa
sababu ya kukuweka benchi hivyo unakua na amani na kujua nafasi yako bado ipo
vile vile tatizo tu ni mipango ajili ya mechi husika, ni mmoja kati ya makocha bora sana hapa nchini”alimalizia
.
 |
| KOCHA JUMA MWAMBUSI |
Seth ambae ni bingwa wa kupiga chenga na
kubadili muelekeo kila anapoona njia zimeziba, amesema ana matarajio ya kujifua
sana wakati huu wa mapumziko ili awe mzuri zaidi katika duru la pili….hawakukosea
kumwita jina la Messi…..
No comments:
Post a Comment