IVORY COAST YAINGIA KOMBE LA DUNIA
Goli lililofungwa dakika za nyongeza
na Salomon Kalou lilitosha kuwapa
nafasi Ivory Coast kuungana na Nigeria
kutinga katika kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Katika mchezo wa kwanza Ivory Coast walitoka na ushindi
wa magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa jijini Abidjan Ivory Coast.
Senegal walikua wa kwanza kupata bao
baada ya mshambuliaji
wa Ivory Coast Didier Drogba kumfanyia faulo
mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane na mwamuzi kuamuru ipigwe penati na Sow
akaikwamisha wavuni na kuwafanya Senegal wawe mbele kwa goli moja.
Senegal walihitaji goli moja ili iwe
2-0 na wapite kwani wangekua na faida ya goli la ugenini, na dakika 15 za
mwisho walishinda golini mwa Ivory Coast na kufanya mashambulizi mengi ya nguvu
lakini kipa Boubacar Bary alijitahidi kuokoa.
Katika dakika za majeruhi
Senegal walifanya shambulizi kali na kupata kona lakini Salif Sane akakosa goli
la wazi na mpira ulivyorudi upande wao Yaya Toure alitoa pasi nzuri kwa Salomon
Kalou aliyefunga na kuamsha shangwe nchini Ivory Coast.
Mchezo huo ulichezwa jijini
Casablanca Morocco badala ya nchini Senegal baada ya nchi hiyo kufungiwa
kutumia viwanja vyake kutokana na vurugu.
Ivory Coast imeungana na Nigeria na kua
timu ya pili toka Africa kutinga katika kombe la dunia litakalofanyika nchini
Brazil.





No comments:
Post a Comment