Manow
ni moja ya sehemu tulivu na yenye uoto mzuri wa asili na mazingira yake
ni mazuri mno nay a kupendeza. Ipo katika wilaya ya Rungwe, karibu kabisa na
mlima Kyejo, mlima ambao una volcano
iliyokufa. Manow pia iko katika sehemu
inayopatikana gesi ya ukaa (carbon dioxide) ambayo inatumika katika ukanda wote
wa Afrika mashariki na kusini.
 |
| MANOW |
Manow ipo kilomita 47 toka Tukuyu mjini
na ukitokea Mbeya mjini ni kilomita 120. Ni sehemu ambayo inapendeza sana na
mandhari yake inakufanya upende kuendelea kukaa.
 |
| MLIMA KYEJO |
Kuna baridi muda wote wa mwaka, ni
nadra sana kwa miezi mingine hata kuliona jua, Mvua inayesha zaidi ya nusu ya
mwaka, hivyo kufanya wakulima walime mwaka mzima , na uzuri wa Manow,hakuna zao
linalogoma kuota labda yanayoota pwani tu ila kila kitu kinakubali. Na kwa vile
ardhi yake ina rutuba sana mazao kama karoti, viazi,ndizi,matunda ya aina zote,
mahindi, maharage ,maparachichi (makatapera) na kila aina ya mazao yanaota
vizuri sana.
 |
| LWANGWA |
Kinachofurahisha zaidi, hakuna magonjwa
ya kuambukiza Manow, magonjwa kama
Malaria na Typhoid hayapo kabisa na
ukiona mtu anaumwa ugonjwa huo jua amekuja nao toka sehemu nyingine. Pia maji
yake ni safi na salama haina haja ya
kuyachemsha, vyanzo vya maji ni salama na
visafi hivyo hakuna hatari kama sehemu nyingine za Tanzani.
 |
| MBIGIRI |
Kuna shule nzuri ya Manow ambayo ipo
kidato cha kwanza hadi kidato cha sita, ni shule ya mchanganyiko, wavulana na
wasichana , na ni nzuri kutokana na majengo na pia ni nzuri kwa ubora wa elimu
wanayoitoa,shule hiyo inamilikiwa na kanisa la KKKT dayosisi ya konde, na hilo
linazidisha umakini wa elimu inayotolewa na kupokelewa hapo shuleni.
 |
| SHULE YA MANOW |
Watu wengi toka mkoa wa Mbeya na sehemu nyingine za Tanzania na nje ya Tanzania wamesoma katika shule hii ya Manow.
 |
| MANOW SEKONDARI |
Mandhari ya Manow ni ya kupendeza sana,
Asubuhi kunakua na ukungu ambao unazidi
kupendezesha na pia, Mlima Kyejo ni moja ya sehemu zinazovutia sana kuzitama, Manow
ni sehemu nzuri, safi na inavutia sana, ni moja ya sehemu zinazovutia sana
Tanzania.
No comments:
Post a Comment