Sunday, 24 November 2013

Arsenal yazidi kupaa

Arsenal wamezidi kujikita katika uongozi wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuwafunga Southampton kwa magoli 2-0, magoli hayo yote yalifungwa na Olivier Geroud moja kila kipindi.

       Alifunga goli la kwanza kutokana na makosa aliyofanya kipa wa Southampton Artur Boric, aliyerudishiwa mpira na beki wake na kutaka kumpiga chenga na ndipo Geroud akawa mjanja na kuuchukua mpira huo na kumpiga chenga  na kisha kuutumbukiza golini.




 
Southampton nao walishambulia wakitafuta goli la kusawazisha na kipa wa Arsenal Woljiech  Szczesny  alifanikiwa kuokoa hatari golini mwake baada ya mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez kutaka kufunga kwa tik tak dakika tano kabla ya mapumziko.

         Kipindi cha pili Southampton walicheza vizur zaidi na Rodriguez na Pablo Osvaldo walikosa magoli  baada ya kupata nafasi nzuri.

      Arsenal nao walifanya shambulizi kali na Theo Walcot alikosa bao la wazi katika dakika ya 82 baada ya kupiga shuti kubwa lililotoka nje ya uwanja.

           Arsenal wallipata goli la pili kwa njia ya penati mwishoni mwa mchezo baada ya beki wa Southampton Jose Fonte kumfanyia madhambi mchezaji wa Arsenal Per Mertesacker na Oliver Giroud akafunga penati hiyo.

 

No comments:

Post a Comment