Saturday, 23 November 2013

Everton yaibana liverpool

          Timu ya Everton imeibana Liverpool kwa kutoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo mgumu na wa kuvutia uliofanyika katika uwanja wa Goodison Park.
Huu ni mchezo uliotoa magoli mengi katika mchezo uliozikutanisha timu hizo toka mwaka 1935.
        Iliwachukua dakika tano kwa Liverpool kupata bao la kwanza


 lililofungwa na Coutinho akiunganisha kona iliyopigwa na Gerrard.Goli hilo lilichangiwa sana na uzembe wa mabeki kushindwa kujipanga vizuri.

      Everton walisawazisha dakika tatu baadae kupitia kwa Mirallas baaada ya Martin  Skrtel kushindwa kuzuia faulo iliyopigwa na Leighton Baines.

       Luis Suarez aliongeza  bao la pili baada ya kupiga faulo ya chinichini  na kumpita kipa wa Everton Tim Howard.Faulo hiyo ilipatikana baada ya Gareth Barry kumfanyia madhambi Suarez.

         Suarez baadae alifanyiwa faulo mbaya na Mirallas lakini mwamuzi akampa kadi ya njano badala ya nyekundu kama wengi walivyofikiria.

        Katika mchezo uliozikutanisha hizo timu msimu uliopita, Mirallas nae alifanyiwa faulo mbaya na Suarez na ilionekana kama vile analipiza kisasi.

            Everton walisawazisha kupitia kwa Lukaku baada ya kupokea mpira toka kwa Mirallas ambae aliwasumbua sana mabeki wa Liverpool. Kabla ya goli hilo, kipa wa Liverpool Mignolet aliweza kumzuia mara tatu mshambuliaji huyo hatari wa Everton.

           Baadae Lukaku akafunga goli la tatu  kwa kichwa akiunganisha kona iliyopigwa na Mirallas, ambae alicheza vizuri sana katika mchezo huo-ukiondoa faulo aliyomfanyia Suarez.


        Lakini Liverpool  hawakukata tamaa na wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Sturridge, aliyeingia mwishoni na ambae hakuanza kutokana na kutoka kupona majeraha aliyoyapata katika timu ya taifa, na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa magoli 3-3

No comments:

Post a Comment