Wayne Rooney aliifungia Manchester United goli la kuongoza
, lakini mchezaji wa zamani wa Manchester United Frazer Campbell akaisawazishia Cardiff .
Baadae Rooney akapiga kona iliyomkuta Patrice Evra aliyepiga kichwa na kufunga
goli la pili, Cardiff wakasawazisha tena kupitia kwa mchezaji aliyeingia
kipindi cha pili, Kim aliyefunga kwa kichwa sekunde chache kabla ya mchezo
kumalizika na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa magoli 2-2.
Rooney alikua na bahati ya kuendelea na mchezo huo kwani alimfanyia faulo mbaya mchezaj wa Cardiff Mutch lakini akapewa kadi ya njano na kutoa ahueni kwa mashabiki wa United.
Campbell angeweza kuongeza goli pale
mpira aliopiga ulipogonga mwamba wa goli na kurudi uwanjani.
Katika dakika za mwisho United walipoteza
nafasi kadhaa za kuweza kushinda mchezo huo, mbili alipoteza Danny Welbeck
baada ya kubaki na golikipa na kushindwa kufunga, na moja aliipoteza Wayne
Rooney bada ya kupiga kisigino ili kumpa pasi Welbeck badala ya kufunga yeye
mwenyewe.
United hawakkucheza vizuri katika
kiungo na hvyo kumfanya kocha David Moyes awe na kazi kubwa ya kufanya maana
hata mchezaji Maloune Fellaini bado hajatoa msaada mkubwa kama ilivyotegemewa.





No comments:
Post a Comment