ARSENAL BALAA
yaifunga Cardiff 3-0
Aaron
Ramsey alifunga magoli mawili dhidi ya timu yake ya zamani ya Cardiff katika
ushindi mnono wa magoli 3-0 walioupata Arsenal.
Ramsey ambae kwa sasa yupo katika
iwango kizuri alifunga goli la kwanza kwa kichwa katika dakika ya 29 baada ya
kupokea krosi toka kwa Ozil na kupiga kichwa na mpira kumshinda kipa aliyekua
kasogea mbele.
Goli hilo lilishangiliwa na mashabiki wa
timu zote mbili, wa Arsenal na wa
Cardiff timu ambayo Ramsey aliihama mwaka 2008 na kujiunga na Arsenal.
Kabla ya hapo, Olivier Giroud
alikosa goli la wazi pale alipobaki na kipa wa Cardiff baada ya kupokea pasi
nzuri sana ya Ozil lakini akasita kuupiga mpira akidhani ameotea na hadi
alipoamua kupiga tayari akawa amechelewa.
Cardiff walijitahidi kutafuta bao
la kusawazisha na walikosa nafasi mbili nzuri moja akiikosa Campbell alipopiga
kichwa na kipa wa Arsenal akautoa nje na nyingine nzuri ni kichwa kilichopigwa
na Ben Turner lakini mpira ukatoka juu kidogo ya goli.
Ramsey aliongeza bao la tatu katika
dakika za majeruhi baada ya kuupata mpira uliookolewa kutokana na shambulizi
lililofanywa na Cardiff.






.jpg)
.png)
No comments:
Post a Comment