Man u
yachapwa
Manchester United imefungwa kwa
mara ya pili mfululizo katka uwanja wa nyumbani wa Old Traford, kwa goli
lililofungwa na Yohane Cabaye katika dakika ya 61, na kuifanya Newcastle United
kuishinda Manchester United kwa mara ya
kwanza katika uwanja huo toka mwaka 1972.
United hawakucheza vizuri katika mchezo
huo, kwani hakukua na mpango mizuri ya kutafuta goli na haikushangaza hadi
kipindi cha kwanza kinakwisha walikua wamefanya shambulizi moja tu langoni mwa
Newcatle.
Kipindi cha pili angalau kidogo
walishambulia pale kichwa kilichopigwa na Patrice Evra kiliokolewa na Anita
katika mwamba wa goli, na pia Robin Van
Persie aliweza kutumbukiza mpira golini lakini ikawa ni off side.
Newcastle walipata goli lao la ushindi
kupitia kwa Yohan Cabaye aliyepokea krosi toka kwa Mousa Sissoko ambae alifanya kazi nzuri
ya kumpita Patrice Evra.
Kwa matokeo hayo Man imepoteza point 13
hadi sasa katika uwanja wake wa nyumbani, hali iliyowafanya mashabiki wengi
watoke uwanjani kabla hata mchezo haujaisha.






No comments:
Post a Comment