Cameroon ndani kombe la dunia
Cameroon wamepata ushindi mnono
wa mabao 4-1 dhidi ya Tunisia na kujihakikishia nafasi ya kushiriki kombe la
dunia litakalofanyika nchini Brazil 2014.
![]() |
| JEAN MAKOUN |
Walipata goli la kwanza mapema kabisa
katika dakika ya 3 ya mchezo lililofungwa na Piere Webo baada ya kumpokonya mpira beki wa Tunisia Karim Haggui na kupiga shuti kal
la chini la kushoto lililompita kipa wa Tunisia na kuingia golini.
![]() |
| MAKOUN AKIMTOKA MLINZI WA TUNISIA |
Moukandjo aliipatia Cameroon bao la pili
katika dakika ya 31 baada ya kuwapita mabeki watatu wa Tunisia na kupiga mpira
ulioingia pembeni na kuhesabu goli la pili.
Akaichi aliipatia timu yake ya Tunisia
bao baada ya kuunganisha kwa mguu wa kushoto baada ya kumzidi mbio mlinzi wa Cameroon
Aurelion Chedjou.
Makoun aliipatia Cameroon bao la tatu kwa
kichwa baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Assou Ekoto .na baadae akafunga goli la nne na la
mwisho na kuwahakikishia Cameroon nafasi ya kucheza katika kombe la dunia.
Cameroon wamekua nchi ya tatu kufanikiwa wakizifuata timu za Nigeria na
Ivory Coast zilizokwishapita.





No comments:
Post a Comment