UHURU ARUDI SIMBA
Uhuru Selemani amerudi katika
timu ya Simba baada ya kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkopo.
Ni mmoja kati ya wachezaji wenye kipaji
cha hali ya juu sana cha soka, anaeweza kucheza kama kiungo wa pembeni, na pia
ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mshambuliaji,
Sifa yake kubwa ni uwezo alio nao wa
kupiga chenga za kwenda mbele, na kupiga mashuti kwa miguu yote miwili, pia ana
uwezo mkubwa wa kupiga shuti huku anakimbia, hivyo mara nyingi anawapa taabu
sana mabeki wanaojaribu kumzuia.
Akiongelea kuhusu kurudi kwake
katika timu ya Simba Uhuru alisema “zimebaki
hatua chache sana kwangu mimi kurudi Simba,na mimi binafsi sina kipingamizi
chochote, kwani pale ni nyumbani na napata faraja kuona bado nina uwezo wa
kuitumikia timu yangu ya Simba,hivyo nipo tayari kuitumikia Simba”
Hongera Uhuru tunasubiri kuona vitu vyako adimu.

.jpg)


No comments:
Post a Comment