Deus kaseke
Engine ya mbeya city
Ana kasi ya ajabu, anazunguuka uwanja
mzima , anapiga chenga na kutafuta
nafasi kila muda anaokua hana mpira, Si
ajabu hadi leo mashabiki wa Simba bado wanamzungumzia, kwani aliwasumbua viungo
na walinzi wa timu hiyo kupita maelezo
.
.
Alizaliwa Nzovwe jijini Mbeya na kuanza
kucheza soka toka akiwa shuleni, na hata alipofika sekondari katika shule ya
Kalobe alikua ni mchezaji wa kutumainiwa wa timu ya shule.
![]() |
| DEUS KASEKE(pich na deus kaseke) |
Wakati akisoma alikua pia akiichezea timu
ya African Boys ya Nzovwe, na hapo ndipo kipaji chake kilipozidi kuimarika
kwani alikuta vijana weng ambao pia walikua na kipaji cha soka na kuifanya timu
hiyo kua moja kati ya timu nzuri jijiniMbeya.
Alipomaliza sekondari akachukuliwa na
timu ya Polisi Iringa (ambayo sasa ni Lipuli)na akacheza kwa muda kisha
baadae ndipo akafuatwa na kocha Juma Mwambusi na kujiunga na timu ya Mbeya
City.
![]() |
| DEUS KASEKE |
Pamoja na ushindani alioukuta katika
timu hiyo, hua anapata nafasi mara kwa mara, na mara nyingi amechezeshwa kama
kiungo mshambuliaji anaetokea pembeni, iwe upande wa kushoto au kulia, ingawa
hua anazunguuka uwanja mzima.
Amekua ni kama injini ya timu kwani
magoli mengi hua yanatokea upande wake, iwe kwa kupiga pasi ya mwisho au hata
kuanzisha move ya goli.Ni mzuri sana
hasa anapobakia na beki mmoja au wawili, hua anawamaliza kirahisi hadi
mtazamaji anaona kama wanafanya makusidi kupitwa.
![]() |
| DEUS KASEKE AKIWATOKA AGREY MORIS NA HUMPHREY MIENO WA AZAM |
Katika sare ya magoli 2-2 na Simba
alimsumbua sana mlinzi wa kushoto wa Simba Issa Rashid baba ubaya kiasi mchezo
ulipokwisha aliyekua kocha wa Simba alimlaumu mno huyo beki kua ndie
aliyesababisha hiyo sare,kwani alikua anapitwa kirahisi na Deus.
![]() |
| DEUS AKIMUACHA WAZIR SALUM WA AZAM |
Hata katika mchezo wa mwisho wa raundi ya kwanza dhidi ya
Azam,aliwafanya mabeki Erasto Nyoni, Said Morad,Waziri Salum na Agrey Moris washindwe
kabisa kumzuia,kwani alikua akiwapita anavyotaka, hata goli la kwanza
lililofungwa na Mwegane Yeya alipiga krosi mbele ya Nyoni huku wakiwa
wamesimama na wanatazamana.
![]() |
| DEUS AKIINGIA NDANI YA BOX HUKU AKITAZAMWA NA AGREY NA SAID MORAD |
Deuse Kaseke ni mmoja kati ya wachezaji
ambao wana nafasi kubwa sana ya kufanya mabadiliko ya soka nchini Tanzania,
haitakua ajabu kusikia kapata timu na kwenda kucheza nje ya nchi, kwani kiwango
chake ni kikubwa sana kwa ligi ya Tanzania.






No comments:
Post a Comment