RONALDO AIPELEKA URENO BRAZIL
Ronaldo akiwa katika kiwango
chake bora kabisa amefanikiwa kuisaidia nchi yake kuingia katika fainali za
kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Katika mchezo wa kwanza Ureno walishinda
kwa goli moja lililofungwa na Ronaldo,hivyo walikwenda Sweden wakiwa na faida
ya hilo goli.
Kipindi cha kwanza hakukua na goli
lolote na kasi ilikua ni ndogo lakini mambo yalikuja badilika katika kipind cha
pili,Ronaldo alikua wa kwanza kuipatia timu yake goli la kwanza katika dakika
ya 50.
Ibrahimovic alisawazisha kwa kichwa kufatia kona iliyopigwa na Kim Killstrom na
kurudisha matumaini ya kuendelea.
Ibrahimovic alifunga tena goli la pili
baada ya
Lakini furaha ya wasweden ilikazimwa tena na
Ronaldo aliyefunga goli la pili baada ya kupokea mpira toka kwa Almeida na
kupiga shuti lilitinga wavuni.
Hakuishia hapo kwani alifunga goli la
tatu baada ya kumpiga chenga kipa wa Sweden na kisha kufunga goli la tatu
lililowapeleka Ureno hadi katka fainali za kombe la dunia.hadi mchezo unakwisha
Ureno 3 na Sweden 2.
Kwa ujumla ilikua ni kama vta ya
Ronaldo na Ibrahimovic,kwani macho yaw au wote yalikua yakiwatazama wao, na kwa
mchezo wote wameonyesha mchezo wa hali ya juu sana na kufunga magoli muhimu,
ingawa Ronaldo ndio anaondoka na ushindi maana tmu yake imefanikiwa kushinda.






No comments:
Post a Comment