Saturday, 9 November 2013

Juma mwambusi
Kocha aliyeleta mabadiliko ya soka Tanzania

  Sasa hivi kila kona ya Tanzania kinachozungumzwa sana kwa mashabiki wa soka ni juu ya timu ya Mbeya  City.  Na cha kufurahisha kila mmoja
anaongelea jinsi wanavyotandaza  soka  maridadi na kuzipa shida timu zote ilizokutana nao.
       Walipoanza ligi ilionekana kama ni  timu ya kawaida kama nyingine ilizopanda nazo daraja,  Ashanti na Rhino, lakini kila ligi inavyoendelea  ndivyo ubora wa Mbeya City unazidi  kuonekana,kwani katika michezo kumi na tatu iliyocheza hajafungwa hata mara moja, na imeweza kumaliza mzunguko wa kwanza ikishika nafasi ya tatu, wakipishana kwa magoli tu na timu ya Azam iliyo nafasi ya pili.
             Mafanikio ya timu hiyo yanatokana hasa na umahiri wa kocha anaefundisha timu hiyo, Juma  Mwambusi, ambae amefanya kazi inayoonekana na kila mpenda soka wa Tanzania.
    Akiongelea mafanikio ya timu hiyo kocha Mwambusi amesema  “Tulichofanya kwanza ni kutafuta vipaji vya hapa hapa nyumbani,na kwa vile kuna mashindano mengi yanayofanyika jijini Mbeya ilikua ni rahisi kuwafatilia walipokua wakicheza mara kwa mara,hivyo hadi kufikia kumsajili unajua kabisa ana uwezo gani na anacheza vizuri sehemu gani, Pili tulianza matayarisho mapema  na kuwafanya wachezaji wazoeane sana kabla hata ligi haijaanza, na hilo limetusaidia, kwani kila mchezaji akipata nafasi anacheza kwa kiwango kile kile ambacho wengine wanacheza.
KIKOSI CHA MBEYA CITY

             Na jambo la tatu ambalo ni kubwa zaidi, nilisisitiza kusajli wachezaji wenye nidhamu,ambao bado wana kiu ya mafanikio na inakua rahisi hata kuwafundisha na kufata maelekezo.Ndio maana unakuta timu yangu wachezaji wana nidhamu na wanajituma toka mwanzo hadi mwisho.”
Ingawa hakusita kusifia uongozi wa timu hiyo na mashabiki wake.    “Viongozi wa timu yetu wanafanya kazi kubwa sana kujaribu kutimiza kila tunachohitaji na wanatusikiliza kila tunapokua na matatizo,lakini pa mashabiki wa timu hii ni mfano wa kuigwa,nawashukuru sana wanavyojitolea,wanasafiri kila mahali tunapokwenda kucheza na wanashangilia mwanzo had mwisho,hata tukianza kufungwa bado wanaendelea kushangilia kwa nguvu ile ile,wanafanya kazi kubwa sana,sisi kama wachezaji tuna deni kubwa sana la kuwalipa hao mashabiki na kikubwa ni kujituma kwa nguvu na kujitolea ili tupate ushindi”
MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKISHANGILIA KABLA YA MECHI NA AZAM
       Akiongelea kuhusu mchezo wa mwisho walocheza na timu ya Azam alsema “kuna mapungufu ya maamuzi lakini hilo si la kusema sana kila mtu aliona ila  kikubwa kilichotokea ni kwa vile vijana wangu hawakuzoea kucheza katika nyasi bandia,tulifanya mazoezi kidogo  uwanja wa Karume siku moja kabla ya mechi, lakini kwa siku moja huwezi kuzoea,ndio maana utaona hata goli la tatu beki wetu aliteleza kutokana na nyasi hizo.”
MOJA YA MABASI YALIOLETA MASHABIKI WA MBEYA CITY KUCHEZA NA AZAM
         “Watu wengi hawakuamini kama tutafika hapa tulipofika,wengi walijua  ni nguvu ya soda, lakini sasa hivi kauli zao zimebadilika,ninajivuna kwa vile nina kikosi kikubwa,wanaocheza ni 11 lakini wapo wengine nje zaidi ya 18 wana uwezo sawa sawa na hawa wanaocheza, ndio maana hata mabadiliko nikifanya anaeingia anafanya vizuri kama aliyetoka,mfano mwanzoni alikua akifunga magoli Mwegane Yeya,lakini alipokuja kucheza Peter Mapunda nae akatufungia mfululizo magoli muhimu sana na sasa hivi hapa kafunga tena Mwegane,kwa hiyo najivunia sana vijana wangu na kwa njia hii nadhani tutafika sehemu nzuri  ligi itakapofika ukingoni.”



No comments:

Post a Comment