Sunderland yaifunga man city
Manchester City imepoteza mchezo wanne
katika ligi kuu ya Uingereza, baada ya kufungwa goli 1-0 na tmu ya sunderland.
Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa
na Phil Bardsley katika kipindi cha kwanza baada ya kumtoka James Milner na
kuukata ukaingia pembeni mwa goli.
 |
| PHIL BARDSLEY AKIFUNGA GOLI LA USHINDI |
Baada ya kufungwa goli hilo Man city
walilishambuli mfululizo lango la Sunderland, lakini kazi kubwa ilifanywa na
walinzi na golikipa wao Vito Manone, walijipanga vizuri na kuhimili misukosuko
yote iliyokua ikielekezwa langoni mwao.
 |
| PHIL BARDSLEY AKISHANGILIA |
Mlinzi wa Sunderland Wes Brown ambae
alikua nje ya uwanja kwa miezi 22 kwa majeruhi alishirikiana vizuri na beki
mwenzake walietoka nae Manchester United John O’shea kuweza kuwazuia washambuliaji wenye uchu
Sergio Aguero na Alvaro Negredo wasilete madhara.
 |
| WES BROWN AKIPAMBANA NA NEGREDO |
Dakika kumi za mwisho,Man City
walizidisha mashambulizi na Eden Dzeko
allipiga shut lililopanguliwa kwa ngumi na kipa Vito.na baadae Aguero alipiga
shuti lililodakwa na kipa huyo.
 |
| SERGIO AGUERO |
No comments:
Post a Comment