MASHABIKI
WA MBEYA CITY WALIVYO AMSHA AMSHA DAR
Mamia ya mashabiki wa Mbeya City
waliosafiri toka mbeya wameleta burudani kubwa uwanjani katika mchezo wa Azam
na Mbeya City.
Licha ya kua walikua ugenini lakini yeyote aliyeona jinsi
walivyojaa na kushangilia bila kuchoka angeamini walikua wanacheza uwanja wa
nyumbani.
 |
| SHABIKI WA MBEYA CITY GWAKISA NA NYUMA YAKE LORI LILILOLETA MASHABIKI WA KUKODIWA WA AZAM |
Pamoja na timu ya Azam kuleta mashabiki
wa kukodi waliofika uwanjani kwa kutumia magari ya fuso,lakini walishindwa
kuhimili amsha amsha ya mashabiki hao kutoka Mbeya.Kuanzia saa tano asubuhi
walianza kufika kwa makundi na hata walipoambiwa tiketi zimekwisha walizidi
kumiminika na kufanya uongozi wa soka kuuza tiketi za ziada tofati na
makubaliano ya mwanzo.
 |
| SHABIKI WA AZAM ALIYEWATUKANA WATU WA CITY |
Kivutio kikubwa kilikua pale shabiki wa
timu ya Azam ambae alikataa kutaja jina lake alipowafata na kuwatukana akitamba
kwamba hawana uwezo wa kumfanya kitu,alishangaa alipojikuta amezungukwa na
kundi kubwa la mashabiki wa Mbeya City kila mmoja akitaka kumpiga,alikua mpole
na kuomba msamaha lakini baada ya kupata vibao kadhaa huku wenzake wakikimbia
bila ya kumpa msaada.
 |
| AKIPATA KICHAPO |
Kichapo kilipomzidia alilia kwa sauti
kubwa ndipo mashabiki wengine wa Mbeya City walipoamua kumsaidia na kumuondoa
eneo hilo huku akilia kama mtoto.
 |
| WAKIMUONDOA BAADA YA KUOKOLEWA |
Kwa ujumla mashabiki hao
wameshangilia muda mwingi kwa amani na furaha kubwa hata pale timu yao ilipokua
nyuma walizidi kushangilia ili kuwapa moyo.
 |
| SHABIKI MAARUFU TOKA MWANJELWA MBEYA, GWAKISA AKIWA NJE YA UWANJA AKISUBIRI KUINGIA |
Mmoja kati ya hao mashabiki aliyejitaja
kwa jina la Gwakisa toka mwanjelwa Mbeya alisema amekuja kushangilia timu yake
kwa vile anajua ni wazuri hivyo anaona rah asana kuishangilia,alisema ana
uhakika AZAM hawana uwezo wa kuifunga Mbeya City,na ukweli hawajawafunga.
No comments:
Post a Comment