Sunday, 10 November 2013

MAN UNITED MBABE WA ARSENAL


      Toka ajiunge na timu ya Manchester United akitokea  timu ya Arsenal,Robin Van Persie amefanikiwa kuifunga timu yake ya zamani kila wanapokutana nayo,  wamekutana mara tatu na kafunga mara tatu pia.
VAN PERSIE AKIFUNGA GOLI LA USHINDI
         Alifunga kwa kichwa katika dakika ya 27 kufuatia kona iliyopigwa na Wayne Rooney  na kuipa timu yake ushindi muhimu katika wakati mufaka.
      Kwa matokeo hayo, Manchester wamesogea hadi nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, na kuwafanya mashabiki wao kutulia.
VAN PERSIE AKISHANGILIA

     Katika dakika 15 za mwanzo  mpira ulichezwa  sana katikati ya uwanja na  Manchester United walicheza kwa nguvu sana kujaribu kuzuia na kushambulia kila wanapopata nafasi na kuwafanya Arsenal washindwe kucheza mchezo waliozoea.
VAN PERSIE AKIZONGWA NA FLAMINI
         Manchester walipata goli lao katika dakika ya 27 baada ya shambulizi kali lililofanywa na Wayne Rooney na Thomas Vaemaelen akaupiga kichwa na kua kona iliyopigwa na mwenyewe Rooney na Van Persie akapiga kichwa kilichoingia langoni mwa goli la Arsenal.
       Kablaya mapumziko United walipata pigo baada ya beki wake Nemanja Vidic kuumia na kutolewa baada ya kugongana na kipa wake David De Gea wakati akiokoa mpira.
VIDIC AKITOKA BAADA YA KUUMIZWA
          Kipindi cha pili Arsenal walitulia na wakapanga mashambulizi yao vizuri lakini alikua ni Wayne Rooney aliyekosa goli la wazi pale mpira uliopigwa na Van persie ulimkuta Shinji Kagawa nae akampa pasi Rooney aliyepiga kwa mguu wa kushoto na mpira ukatoka nje pembeni kidogo ya goli la Arsenal.

     Hadi mchezo unaisha United walitoka na ushindi wa hilo goli moja.

No comments:

Post a Comment