NJIA 40 ZA
KUISHI KWA FURAHA BILA MAJUTO
FURAHA NI KITU KIKUBWA SANA KATIKA MAISHA,FURAHIA MAISHA
USIWE NA MANUNG’UNIKO WALA MAUDHI MOYONI…..HIZI NI NJIA 40 ZA KUKUSAIDIA KUISHI
KWA FURAHA………
1.ELEWA NA KUKUBALI KWAMBA KUFANYA MAKOSA NI JAMBO LA
KAWAIDA
(kufanya kosa ndio kujifunza)
2.AFYA YAKO IWE MUHIMU KWAKO
(jali afya yako,ukijisikia
uko tofauti japo kidogo nenda katibiwe na wataalam,usinywe dawa kwa mazoea)
3.FATA MAAMUZI YAKO
USIAMULIWE
(kua na msimamo wa unachoona
ni kizuri,usikubali kuburuzwa)
4.JARIBU KUFANYA MAMBO
YATAKAYOKUFURAHISHA,EPUKA YATAKAYOKUKERA
(epuka maudhi,kwani mwisho
wake ni hasira na karaha)
5.KUA MTULIVU,USIHARAKISHE
KUFANYA JAMBO LOLOTE
(chunguza kila kitu kwa makini kabla
hujaamua kukifanya)
6.KUA MDADISI,USIHOFU
KUJARIBU JAMBO JIPYA
(usikubali kufanya kitu kwa
kuelezwa tu kua ni kizuri,uliza unachoona kinakutia mashaka)
7.SOMA SOMA KILA
WAKATI,UPANUE MAWAZO
(kila unaposoma kitu
kipya.akili yako inazidi kutanuka,soma kila unapopata muda)
8.FURAHIA MAMBO NA WATU
TOFAUTI
(jichanganye,usiwe kila mara
mpweke)
9.JIWAZIE KWANZA WEWE
MWENYEWE,
(usiwe unaomba ushauri sana
kuhusu maisha yako fanya moyo unavyokutuma)
10.USIWAHUKUMU WATU KABLA
HATA HUJAWAJUA
(usipende kufikiria ubaya kwa
kumtazama tu mtu sura yake)
11.SHUKURU KWA ULICHONACHO,USIJUTIE
KILE AMBACHO HUNA
(usipokifurahia wakati
unacho,kitakapopotea utaanza kukikumbuka na kujuta kwa nini hujakithamini)
12.FURAHIA MAFANIKIO YA
WENZAKO,USIONE AIBU KUSIFU KISICHO CHAKO
(ufate moyo wako kwa kusifu
kila kilicho kizuri,hata kama si chako)
13.UKIFURAHISHWA NA KITU
WAAMBIE NA WENZAKO,USIFURAHIE PEKE YAKO
(kua na kampan ni bora zaidi
ya kukaa peke yako)
14.USIMSHAWISH MWENZAKO
ABADILIKE ALIVYO,KWANI ALIVYO NDIVYO ALIVYO
(utakapotaka
kumbadili,akigoma mnaweza kua maadui,bora muache kama alivyo)
15.UKIWA SAFARINI FURAHIA
SAFARI,SI KUWAZA UTAFIKA SAA NGAPI
(ukiwaza sana unaweza kuanza
kuona gari haiendi kasi sana na baadae ukaja juta kwa haraka zako)
16.JIZUIE KUWAZA MAMBO
MABAYA,JILAZIMISHE KUWAZA MAZURI
(kwani unavyowaza mabaya kila
muda mwisho utakuja kutenda maovu)
17.ELEWA FURAHA NI JAMBO
KUBWA SANA MAISHANI KULIKO HATA UTAJIRI
(ridhika na furahia na kila jambo lako
ulilofanikisha,japo ni kidogo
18.TUMIA NGUVU ZAKO KWA
UMAKINI,
(usitumie kwa kufanya mambo
ya kijinga.usisikitike,usijute na wala kunung’unika,,,)
19.KUA JASIRI KAMA KUNA KITU
CHA KUBADILI KIBADILI MARA MOJA USISITE
(Usisite kufanya maamuzi
kwani unaweza kuwaza jambo jingine likavuruga wazo zuri la mwanzo)
20.FURAHIA KAZI YAKO
(jali na kuiona kazi yako
unayofanya ni bora kuliko kitu chochote)
21.USIKATE TAMAA,MATATIZO
YAKO YAFANYE YAWE NI CHANGAMOTO YA KUPIGANA ZAIDI
(matatizo
hayakimbiwi,yanatatuliwa)
22.TAFUTA NJIA TOFAUTI
TOFAUTI ZA KUTATUA MATATIZO YAKO,
(usilazimishe njia moja,jaribu
kutafuta suluhisho jingine kama unalotumia unaona halisaidii)
23.KUA HURU UKIAMINI KILA MTU
YUKO HURU
(fanya jambo kwa maamuzi yako
si ya kuambiwa)
24.TANUA MAWAZO KWA KUWAZA
VITU TOFAUTI TOFAUTI
(usiwaze kitu hicho hicho
kila siku,ukikiwaza kitu kimoja unaweza kupata wazimu)
25.USISUMBUKE NA WATU UNAOONA
NI WABISHI KWA KILE ULICHO NA UHAKIKA NACHO
(chunguza wa
kuwaelewesha,kuna wengine wamezaliwa wabishi)
26.KUA MKWELI KWA NAFSI YAKO
NA KWA WENZAKO
(ukiurudia rudia uongo mwisho
unakukaa mawazoni hadi mwenyewe unaamini ni ukweli)
27.JIKUBALI ULIVYO,KWANI
ULIVYO NDIVYO ULIVYO
(ulivyo ndivyo ulivyo,na
alivyo mwingine ndivyo alivyo)
28.HESHIMU KILA
MTU,USIMDHARAU YEYOTE
(fikiria sana kabla ya
kumdharau mtu,ingekua wewe umedharauliwa ingekuaje?)
29.ISHI SASA USIWAZE BAADAE
ITATOKEA NINI
(usiogope sana kuhusu
baadae,utakua huna amani maisha yote)
30.USIAHIRISHE JAMBO FANYA
KWA MUDA
(mwisho wa kuahirisha ni
kutokufanya kabisa)
31.USIWEKE VISASI,SAMEHE MARA
MOJA NA UENDELEE NA MAISHA,
(ukiweka sana
visasi,hutafanya mambo yako kwa amani lakini ukisamehe utakua huru daima)
32.MALIZA TATIZO,USISITE AU
KUWAZA MBELE ITAKUAJE
(mwisho wa tatizo ni furaha)
33.KAA NA WATU WATAKAOKUPA
FURAHA SI MAUDHI
(usikae na watu
wanaotengeneza majungu na fitna)
35.JITETEE MWENYEWE
(hakuna wa kupigana vita yako),,,,
36.JIPENDE
( ukijpenda na watu watakupenda)
37.FANYA KITU
UNACHOPENDA,USIJINYIME
(usiige wanavyofanya watu ili
na wewe uonekane mjanja,fanya unalomudu)
38.ANDIKA MAWAZO NA MALENGO
YAKO
(na uvifanye hatua kwa hatua
na usikate tamaa kama mambo hayaendi vizuri)
39.FANYA VITU VITAKAVYOKUPA
FURAHA
(jitahidi kutoa msaada kila
unapoweza)
40.KILA MARA JITAHIDI KUSONGA
MBELE,
(usiwe unajikumbusha sana
mambo yaliopita…..)
INGAWA NI LISTI NDEFU LAKINI INA MANUFAA
SANA,JARIBU KUCHAGUA MAMBO 18 HALAFU YAFANYIE KAZI NINA UHAKIKA UTAISHI KWA
FURAHA NA AMANI SANA…

No comments:
Post a Comment