YOHANA
MORRIS
STOPPER WA MBEYA
CITY.
Yohana morris ni mmoja kati ya
wachezaji waliofanikisha kuipandisha Mbeya City,ni beki kisiki ambae ana uwezo
wa kucheza namba nyingi bila shida yeyote.ana uwezo wa kucheza beki wa kulia
pembeni au hata kushoto,na pia anacheza bila shida nafasi zote za kati za
ulinzi.
Yohana amezaliwa katika familia
ya soka kwani kaka zake wote walikua ni wachezaji, kuanzia kaka mkubwa ambae ni afisa wa
magereza mororgoro alikua ni mchezaji mahiri wa timu ya magereza, kaka yake mwingine Osward Morris nae amecheza
sana katika ligi kuu ya Tanzania akiwa na timu ya Prisons na sasa hivi ni kocha
msaidizi wa timu hiyo, wakati mwingine ni Henri Morris ambae alicheza kwa
mafanikio katika timu zaPrisons Yanga,Miembeni ya Zanzibar, na baadae Moro United.
Yohana alizaliwa mkoani Morogoro na kupata elimu
yake ya msingi hapo hapo Morogoro,na toka akiwa shule ya msingi alionyesha
uwezo mkubwa sana wa soka na kumfanya muda mwingi autumie kucheza mpira.
Baadae alihamia Mbeya kwa kaka yake Oswardn huko ndipo kocha maarufu Josef Kanakamfumu akamuona na kuvutiwa
na kipaji chake, akaongea na waalimu wa
shule ya Makongo akapelekwa kusoma sekondari pale
Alipomaliza form four akajiunga na
academy moja iliyokua ikiitwa KICK OFF, na huko akashiriki mashindano kadhaa
yakiwemo maarufu ya ROLLING STONE.
Wakati timu ya Mbeya City inaanzishwa, kocha Juma Mwambusi akamwita na kua ni mmoja wa waanzilishi wa timu hiyo, wakaanza toka daraja la tatu lakini bahati
nzuri uongozi ukainunua timu ya RHINO iliyokua daraja la kwanza,hivyo automatic
wakacheza ligi daraja la kwanza lakini bahati mbaya hawakufanikiwa kupanda
daraja,na ndipo msimu uliofata wakajitayarisha vizuri na kufanikiwa kupanda
hadi ligi kuu ya Tanzania. Ameweza kucheza mechi kadhaa na hajawaangusha
wapenzi wa Mbeya City, kwani katika
mechi waliyocheza na Yanga jijini Mbeya alikua ni sumu kwa washambuliaji hatari wa timu hiyo,Kavumbagu na Jerry
Tegete,na hata katika mchezo waliocheza na Simba alifanikiwa kwa kiasi kikubwa
kuwabana washambuliaji wa timu hiyo.
Ukiondoa makosa kidogo yaliyofanywa mwanzoni mwa kipindi cha kwanza na
kusababisha magoli mawili ya haraka toka
kwa Amis Tambwe, aliweza kumshika mshambulaji hatari wa SIMBA Betram Mombeki na
hivyo kuzuia mashambulizi na hatari zote zilizotakiwa kuja katika goli lao….



No comments:
Post a Comment