Arsenal yachezea
Arsenal imepoteza mchezo wa pili
mfululizo baada ya kufungwa na Man City kwa magoli 6-3 katika mchezo ambao
kiungo wa Man City Fernandinho alichaguliwa kua ni mchezaji bora wa mchezo huo.
Ingawa Arsenal ndio walikua wa kwanza
kulishambulia goli la City baada ya Jack Wilshere kupiga shuti lililotoka nje
ya goli katika dakika ya 11, lakini Man City ndio walikua wa kwanza kupata goli
baada ya kona iliyopigwa na David Silva kugongwa kidogo na kichwa na
Martin Demichelis na kumkuta Sergio Aguero aliyepiga na kutinga golini.
City waliendelea kulisakama lango la Arsenal
na Negredo nusura aifungie timu yake baada ya kupewa pasi nzuri na Kompany
lakini akapiga shuti lililotoka nje ya uwanja.
Arsenal walisawazisha baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Aaron Ramsey
baada ya kumnyang’anya mpira Yaya toure na kutoa pasi nzuri kwa Mesut Ozil aliyeingiza mpira ndani na
kumkuta Theo Walcot aliyepiga shuti na kuandika bao.
City waliongeza bao la pili baada ya pasi
kutoka kwa Yaya Toure kumkuta Pablo Zabaleta aliyepiga krosi fupi na Negredo
akakutana nayo na kuifungia City bao la pili.
Wakati wa kujaribu kuokoa hilo
goli beki wa Arsenal Koscielny aliumia na kutolewa.
Goli la tatu la City lilipatikana
baada ya Matheu Flamini kushindwa kuzuia pasi aliyopigiwa na Sagna na
Fernandinho akauvuta na kupiga shuti la kiufundi lililomshinda kipa wa Arsenal.
Arsenal hawakukata tamaa na Walcot aliongeza bao la pili baada ya kazi
nzuri iliyofanywa tena na Aaron Ramsey.
Walikua ni City walioongeza bao baada ya Jesus Navas kupiga
krosi nzuri na Silva alimzidi kasi beki
wa Arsena Mertesacker na kuupiga mpira
na kufunga.
Fernandinho akaongeza bao la 5 baada ya
kuupiga mpira uliomshinda kipa wa Arsenal.
Mertesacker aliongeza goli kwa Arsenal
baada ya kupiga kichwa cha kiufundi na baadae Yaya Toure akafunga goli la 6 kwa
City kwa njia ya penati baada ya kipa wa Arsenal kumfanyia faulo Fernandinho
aliyekua akitaka kufunga.










No comments:
Post a Comment