Saturday, 14 December 2013
Kwa
mwalalika
Mashine ya Mwalalika ipo karibu na shule ya
msingi Itiji, ni sehemu maarufu sana kwa wakazi wa Mbeya,ilianzishwa miaka ya
sitini na mzee Haji Mwalalika,na baadae alipokuja kufariki kwa ajali ya tractor
akiwa pamoja na mwanawe Sadiki mwanzoni mwa miaka ya 80 ikaendelezwa na mwanae mwingine
aliyeitwa Athumani.
Ni mashine iliyokua ikihudumia watu wengi sana kusaga nafaka zao, watu
kutoka Majengo,Ghana na hata Soko Matola walikua wakitegemea mashine hii kusaga
vyakula vyao. Kina mama wengi waliokuwa wakifanya biashara ya pombe za
kiennyeji katika kilabu maarufu cha lejiko nao walikuwa wakijaa sana katika
mashine hii ili kununua pumba za kutayarishia pombe.
kabla ya kuanzishwa kwa mashine hii kulikua na mashine nyingine iliyokua
chini kidogo kuelekea mabatini,ilikua ni ya mtanzania mwenye asili ya kiasia alijulikana
kwa jina la Punja(sijui alitokea sehemu za Punjab India?), ingawa alikua
na jina lake lakini watu wa wakati huo waliamini kipimo chake kilikua kinapunja
na kubakisha unga katika mashine!!!!!ingawa si ukweli bali ni tetesi
zilizozoeleka hadi ikawa kama ukweli,ndipo akapata hilo jina la Punja.nae
alidumu na baadae akawauzia waswahili na ilikuwepo hadi miaka ya tisini
mwishoni.
Kwa wakazi wa Mbeya
watakua wanakumbuka mashine zilizokuwepo miaka ya themanini hadi
tisini,zilikua ni za kuhesabika,ilikua ya Mwalalika,ya Punja na juu kabisa
majengo ilikuwepo ya Bahati,kwa wakati ule zilikua zinafanya sana kazi kwani
viwanda vya kusaga nafaka vilikua bado havijaanza kufanya kazi sehemu kubwa ya
Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment