CHELSEA HOI….
Hull City imepata ushindi mnono
nyumbani baada ya kuwafunga Chelsea kwa magoli 3-2 katika mchezo mzuri uliojaa
ufundi pande zote.
Chelsea walikua wa
kwanza kupata bao lililofungwa na Schuerrle aliyepokea pasi toka kwa Obi Mikel
na kumpiga chenga mara mbili beki wa Stoke City Shawcross kisha kupiga shuti la kiufundi lililomshinda
kipa Begovic.
Stoke
walipata bao la kwanza baada ya kosa lilofanywa na kipa wa Chelsea la kutaka
kutoka na kuamua kurudi hivyo kuwachanganya mabeki na ndipo Peter Crowch
akautuliza mpira na kufunga kirahisi.
Stoke waliongeza bao baada ya Jonathan
Walter kumpita Cezar Azpilicueta na
kutoa pasi kwa Steven Ireland aliyepiga shuti lililokatika na kutinga wavuni.
Lakini Chelsea
wakasawazisha kwa goli lililofungwa tena
na Schuerrle baada ya faulo iliyopigwa na Mata kuokolewa na mpira kumkuta
mfungaji aliyepiga shuti na kuingia golini.
Stoke
walipata goli la ushindi kupitia kwa Oussama Asaidi aliyepokea pasi toka kwa
Ireland na kukimbia na mpira kisha kupiga shuti lililomshinda kipa wa Chelsea na
kuandika goli la tatu.
Hadi mchezo
unakwisha Stoke 3 na Chelsea 2.







No comments:
Post a Comment