Juma ahmad
Kipa wa mecco na tukuyu stars
Alizaliwa Mbeya Soko Matola na kusoma shule ya msingi Mbata mahali
ambapo ndipo alianza kucheza soka kama golikipa, akiwa na watoto wengine wa uswahilini kama kina Allen Simumba,Mbaraka
Kaparata,Amani Masebo na wengine wengi wa soko Matola na maeneo ya Ghana.
Wakati akiwa darasa la saba yeye pamoja wenzake walichukuliwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Said Mkwanda ambae alikua na timu iliyokua maarufu sana jijini Mbeya ya Town Stars huko walikutana na vijana wengine ambao tayari walikua wametangulia kama kina Peter Poka, Juma Songoro “TOZZO” na wengine ambao walikua ni wakubwa kwao kama kina Haji Abas,Kakoko na kina King Kubenda na mchanganyiko wao ulikua ni timu moja iliyokua kali na inatisha sana jijini Mbeya.
Baadae akachukuliwa na timu ya Mecco, na
alishiriki katika kuipandisha daraja toka daraja la pili hadi daraja la kwanza
(sasa ni ligi kuu ya Vodacom)
Mecco alikutana na wachezaji wengi na
kutoka sehemu tofauti za Tanzania, kama kina
Moses Kaniki,Mbaga Mwintiku,
Nasib Abas,George Mangula, Danny Magogo,Nurdin na Abeid Kasabalala na wengine
wengi.
Akatoka MECCO na kuchukuliwa na Tukuyu
Stars iliyokua pia katika ligi kuu na
akacheza kwa mafanikio kwa misimu mitatu.
![]() |
| Juma Ahmad akidaka mpira,nyuma yake Salum Kussi,na Godwin Aswile,mbele Abeid Mziba na Mohamed Kassanda, wakati TUKUYU STARS ilipocheza na YANGA. |
NaTukuyu Stars alikutana na wachezaji wengi wenye vipaji vikubwa sana kama vile kina Mohamed Kasanda,Justin Mtekere,Emanuel Mwambipile,Ikupilika Nkoba na Peter Luis ambao waliifanya timu ya Tukuyu kua ni moja kati ya timu bora sana zilizowahi kutokea nchini Tanzania.
Akiwa Tukuyu Stars aliweza kucheza mechi karibu zote za ligi na kati ya hizo ni pamoja na michezo migumu waliyocheza na timu za Simba na Yanga.
![]() |
| Juma Ahmad akiudaka mpira huku Mohamed Kassanda akimzuia Edward Chumila |
Baadae akahamia Tiger ya Tunduma
alikokaa msimu mmoja na kisha kwenda
Reli ya Morogoro alikokaa hadi anastaafu kucheza soka.
Kwa sasa Juma Ahmad anafanya kazi Gymkhana Dar na pia ni golikipa wa timu hiyo ya Gymkhana.





No comments:
Post a Comment