Kilimanjaro Stars imeshindwa kupata
nafasi ya tatu baada ya kufungwa kwa penati 6-5 na Zambia katika mchezo wa kutafuta
mshindi wa tatu wa mashindano ya CECAFA senior challenge cup.
Hadi muda wa kawaida unamalizika timu
hizo zilikua sare kwa goli moja kwa moja
kwa magoli yaliyofungwa na Ronald Kampamba wa Zambia aliyefunga baada ya
kumtoka beki wa Stars Said Morad na kupiga shuti la chini lililompita kipa wa
Stars Ivo Mapunda.
Mbwana Samata aliisawazishia Stars kwa
goli zuri la kiufundi baada ya kumzunguka beki wa Zambia na kupiga shuti kali la kushtukiza la mguu wa kushoto na kumshinda kipa wa Chipolopolo.
Felix Katongo na Ronald Kampamba
walifunga penati mbili za kwanza kabla ya Mbwana Samatta na Erasto Nyoni nao
kufunga mbili za Stars, kisha Justin Zulu akakosa baada ya kugonga mwamba, na
kwa Stars Himid Mao akafunga.
Captain wa Zambia Bronson Chama
akaifungia Zambia penati ya nne kabla ya Amri Kiemba nae hajafunga ya nne na
kuifanya Stars iwe mbele kwa penati 4-3. Julius Situmbeko akaifungia Zambia
penat ya mwisho na ikabaki moja kwa Tanzania lakini Athman Chanongo akapiga
penati iliyookolewa na kipa wa Chipolopolo Titima.
Baadae zilipoongezwa moja moja Ramadhani
Singano na Rodrick Kabwe wakapata penati zao kabla ya Ivo Mapunda kuokoa penati
iliyopigwa na Konwan Mtonga. Ikabaki kwa Mrisho Ngasa kumalizia lakini nae
penati yake ikaokolewa na kipa wa Zambia.
Kabaso Chongo akaipatia timu yake penati
iliyofuata kisha Kelvin Yondani akapiga penati liyookolewa na kipa wa Zambia na
kuwafanya Zambia kushika nafasi ya tatu kwa penati 6-5.

No comments:
Post a Comment