MAN UNITED YASHINDA
Magoli
mawili ya haraka haraka yaliyofungwa na Dany Welbeck na jingine lililofungwa na Tom Cleverley
yalitosha kuwafanya Man united kupata ushindi katika ligi ya Uingereza baada ya
kupoteza michezo miwili mfululizo.
Antonio Valencia alikua katika kiwango
kizuri na kuisumbua san na ngome ya Aston Villa, kwani alikua akishirikiana
vizuri na Rafael hivyo kuwapa kazi ngumu mabeki wa Villa.
Man
walipata bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Welbeck aliyekutana na mpira uliogonga
mwamba baada ya Rafael kukimbia na mpira na kupiga krosi ya nguvu iliyomkuta Januzaj aliyepiga kichwa na mpira
ukagonga mwamba.
Welbeck aliwahi kuufikia kabla ya mabeki hawajajipanga na na kufunga goli lake la kwanza katika ligi msimu huu.
Kabla ya Villa hawajatulia, beki wao
Nathan Barker alipoteza mpira na ukachukuliwa na Welbeck aliyempelekea Valencia
ambae nae akapiga krosi ya chini chini na mpira kumkuta Welbeck aliyefunga
goli la pili. Hiyo ilikua ni dakika ya 18.
Man waliutawala mchezo na Valencia akawa
tishio zaidi alitoa pasi nyingi za kusababisha magoli lakini zilipotezwa na washambuliaji
wa Man.
Kipa wa Man alikua muda mwingi wa mchezo
hana la kufanya kwani washambuliaji wa Villa hawakua kabisa na madhara na hata
mchezaji wao hatari Christian Benteke alikua hana msaada mkubwa, hadi sasa
amecheza michezo kumi bila ya kufunga goli.
Man walipata bao la tatu katika dakika ya 52 kupitia kwa
Cleverley aliyepigiwa pasi nzuri a Wayne
Rooney.
Darren Fletcher aliingia katika dakika
ya 70 baada ya kutokuwepo uwanjani kwa kipindi kirefu kutokana na maradhi.
Fletcher aliichezea Man mara ya mwisho tarehe 26 december mwaka jana, hivyo alipokelewa kwa furaha na mashabiki wa timu hiyo.







.jpg)


No comments:
Post a Comment