Wednesday, 18 December 2013

MOURINHO; CHELSEA HAINA WAFUNGAJI

    Pamoja kua na washambuliaji mahiri kama Fernando Torres, Samuel Etoo, na Demba Ba, lakini kocha wa Chelsea Mourinho amesema timu yake haina washambuliaji wa kuweza kuwapatia ubingwa.

        Chelsea walifungwa na Sunderland kwa magoli mawili kwa moja katika mchezo wa kombe la ligi(Capital one).

     Chelsea walipata bao lao katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili baada ya Beki wake wa kulia Azpillicueta kukimbia na mpira na kupiga krosi ya chini chini iliyomkuta Lampad akiwa na beki wa Sunderland  Lee Cattermole na wakaugonga mpira lakini ukoakolewa na kipa ukiwa umepita kidogo mstari wa goli.goli hilo alikuja kupewa Cattermole.

       Chelsea baada ya kupata hilo bao waliendelea kushambulia na baadae beki wa Sunderland Craig Gardner alikosea na kupiga pasi iliyomkuta Etoo lakini akashindwa kufunga baada ya kuupiga mpira nje.
         Sunderland walisawazisha zikiwa zimebaki dakika mbili mpira kumalizika baada ya mpira aliopiga Altidore  kuokolewa vibaya na kumkuta Borini aliyepiga shuti lililomshinda kipa wa Chelsea.

    Katikati ya mchezo huo mtu mmoja ambae alikua amevua shati lake aliinia kati kati ya uwanja na kuufanya mchezo huo kusimama kwa muda.

     Sunderland waliongeza bao la pili zikiwa zimesalia tena dakika mbili za nyongeza wakati Borini alipotoa pasi nzuri kwa Ki aliyejitengenezea nafasi na kupiga shuti lililoingia golini na kuwafanya Chelsea watolewe katika kombe la ligi.


       Akiongea baada ya mchezo huo kocha wa Chelsea Jose Mourinho alisema tmu yake imekosa washambuliaji wenye uchu ndio maana hawapati magoli. 


     Katika magoli 32 yaliyofungwa na timu hiyo  katika ligi ni magoli matano tu yaliyofungwa na washambuliaji. Demba ba kafuga moja, Samuel Etoo kafunga mawili na Fernando Torres nae kafunga mawili.

No comments:

Post a Comment