Stoke hoi kwa man utd
MAN united imefanikiwa kuingia
katika nusu fainali ya kombe la ligi(capital one)baada ya kupata ushndi wa goli
2-0 dhidi ya timu ngumu ya Stoke City.
Katika mchezo huo uliochezwa huku kukiwa
na hali mbaya ya hewa kutokana na mvua na upepo mkali uliokua ukiambatana na
barafu,man walipata mabao yake yote mawili katika kipindi cha pili cha mchezo
huo.
Mchezo ulisimamishwa dakika ya 29 baada
ya hali ya hewa kuzidi kua mbaya na mwamuzi wa pambano kuamua kuusimamisha
mpira hadi hali itakapotulia.mchezo ulisimama kwa dakika kumi.
Goli la kwanza lilifungwa na Ashley
Young katika dakika ya 62 baada ya faulo iliyopigwa haraka haraka na Cleverley
na Young akampasia Chicharito aliyemrudishia Young na akapiga shuti kali sana
lililomshinda kipa wa Stoke.
Young alishngilia sana goli hilo kiasi akaaumua kwenda kushangilia na mashabiki, hali iliyosababisha muamuzi kumpa kadi ya njano.
Stoke nao hawakukata tamaa kwani
walishambulia goli la Man wakiongozwa na kiungo wao makini Steven Ireland, lakini beki ya Man ikiongozwa na Chriss Smalling na
John Evans walikua wakifanya kazi nzuri ya kuzuia mashambulizi hayo.
Jonathan Walters wa Stoke alifanikiwa
kuwapita mabeki wa Man lakini shuti lake lilikamatwa na kipa David De Gea.
Man walipata bao la pili kupitia kwa
beki wao Patrice Evra aliyeingia katia 18 ya Stoke na kupiga mpira mzuri kwa
kutumia mguu wa kuli na kuweza kuandika goli la pili.
Kwa matokeo hayo Man United watakutana na
timu ya Sunderland katka nsu fainali ya mashndano hayo.










No comments:
Post a Comment