Sunday, 26 January 2014

RHINO HOI KWA SIMBA

TIMU YA Rhino  ya Tabora imeshindwa kutamba mbele ya Simba baada ya kufungwa kwa goli moja kwa bila katika mchezo ligi kuu ya Vodacom Tanzania uliochezwa katika uwanja wa taifa Dar es salaam.
WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHANGILIA GOLI LA SINGANO HUKU RHINO WAKILAUMIANA

   Goli la Simba lilipatikana mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wa timu hiyo Ramadhani Singano aliyepiga shuti kali baada ya kukutana na mpira uliiokolewa vibaya na mabeki wa Rhino kutokana na kiki ya Ally Badru.
ALLY BADRU AKIPIGA SHUTI 
      Kwa ujumla muda mwingi mchezo ulikua wa taratibu ingawa ni Simba ambao walipanga mashambulizi mengi langoni mwa Rhino,  lakini hawakuweza kumpita kirahisi kipa wa timu hiyo aliyeokoa hatari kadhaa ikiwemo penati iliyopigwa na Ramadhani Singano
SIMBA WAKISHANGILIA
      Penati hiyo ilitokana na beki wa Rhino kuushika mpira uliokua ukielekea golini kufuatia shuti lililopigwa na Haruna Chanongo.
         Amisi Tambwe aliweza kufanikiwa kufunga mara mbili lakini mwamuzi mara zote akikataa , mara ya kwanza aliunganisha krosi iliyopigwa na Singano lakini wakati mwamuzi akiashiria kua ni goli, msaidizi wake alilikataa, na mara ya pili aliusindikiza mpira uliomshinda kipa lakini pia mwamuzi akasema kuna madhambi yalifanyika.
SINGANO AKIMTOKA BEKI WA RHINO
       Pamoja na Singano kufunga hilo goli moja, lakini alipoteza nafasi nyingi sana za kufunga kutokana na uhodari wa kipa au kutokua makini.

      Kocha wa Simba Loga alimuingiza Betram Mombeki na baada ya kucheza kwa dakika sita akaamua kumtoa kwa sababu alikua amekosea mara tatu na nafasi yake ikachukuliwa na Henry Joseph, jambo lililozua malalamiko toka kwa mashabiki kwamba kocha hajamtendea haki Mombeki.        

No comments:

Post a Comment