Kila la kheri mbeya city…..OBJECTIVE TO WIN
JUMAPILI tarehe 2 february 2014,
Mbeya City wanapambana na Yanga, ni mechi ngumu kuliko michezo yote ambayo
Mbeya City imecheza hadi sasa, Kwa sisi wakazi wa Mbeya tunaitakia kila la
kheri timu yetu ya Mbeya City iweze kushinda mchezo huo.
Tunaamini kikosi chini ya kocha wetu Juma mwambusi na msaidizi wake Maka
Mwalwisi kitafanya vizuri , kwani matayarisho yamekwenda vizuri. Kocha Juma
Mwambusi anasema kila kitu kinaenda sawa, na hata golikipa David Buruan aliyekua
na kadi anatarajia kumchezesha, pia mshambuliaji wake Mwagane Yeya tayari
amepona maumivu yaliyokua yakimsumbua hivyo anatarajiwa kuwemo katika jeshi
litakalopambana hiyo jumapili.
Mashabiki wa Mbeya City nao wameahidi
kutoa mshikamano mkubwa katika mchezo huo, Mwenyekiti wa mashabiki wa Mbeya
City jijini Dar Es Salaam Edwin Mwasenga
anasema wamejipanga kuipa sapoti kubwa timu ya nyumbani, na wametayarisha
usafiri kutoka Ubungo Terminal hadi
uwanjani na kurudi ili kuwapa urahisi mamia ya mashabiki wanaotoka Mbeya kuja
kuitazama timu yao. Anasema kwa jinsi anavyoiamini Mbeya City anatarajia kuwa
watafanya vizuri katika mchezo huo.
![]() |
| MWENYEKITI WA MASHABIKI WA MBEYA CITY JIJINI DAR, EDWIN MWASENGA. |
Nae katibu wa mashabiki hao wa Mbeya City
Njajile anasema wanatarajia kushinda katika mchezo huo, ila wamejipanga hata
kama matokeo yatakua tofauti hawataacha kuipa sapoti kubwa timu ya nyumbani.
Nae mdhamini mkuu wa mashabiki hao Jonson
Lyombe,anasema wamejipanga kuwapokea na kuwarahisishia mashabiki wanaotoka
jijini Mbeya kwa usafiri na kuwaepusha na vurugu za kukata tiketi, hivyo
anashauri wapitie hapo Ubungo Terminal ili iwe rahisi kuwaunganisha na mashabiki
ambao tayari wamekwishafika jijini Dar.
John Mwakalebela nae anasema haoni sababu ya Yanga kuwafunga City, kwani walichopishana ni kwamba Yanga wanacheza sana katika magazeti, ila ukiwaona uwanjani ni wa kawaida sana. Ila hakusita kusema anaogopa sana fitna za nje ya uwanja na waamuzi kupendelea upande pinzani.
![]() |
| JOHN MWAKALEBELA. |
Mmoja wa mashabiki hao aliyetokea Kijiweni
Mwanjelwa Mbeya aliyejitambulisha kwa
jina la Ntoli Mwambusi anasema anafuatilia mechi zote inazocheza Mbeya City,
hivyo amekuja kuitazama timu anayoipenda na inayofanya vizuri ikifanya mambo
yake, akimaanisha ikishinda, hivyo anasema anaamini kesho lazima watashinda,
idadi ya magoli hajajua ila ushindi ni lazima.
| MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIOTOKA KIJIWENI MWANJELWA MBEYA, |
Nae Hance Mfikemo ambae pia
ametoka Kijiweni Mwanjelwa anasema siku zote Mbeya City inamfurahisha, hivyo
anaamini hata kesho watamfurahisha watakapoifunga Yanga. Mboka Mwambusi anasema
hana wasiwasi na timu yake kwani anajua lazima itafanya inalofanya vizuri kila
siku……Ahazi Mfikemo yeye alisema anachosubiri ni muda ufike ili ashangilie
kwani anaamini timu yake itamfurahisha ndio maana kafunga safari toka Mwanjelwa
Mbeya hadi Dar…….kila la kheri Mbeya City………


No comments:
Post a Comment