Anthony matogoro
Mpiganaji wa mbeya city
Mmoja
kati ya wachezaji wanaotamba katika timu ya Mbeya City ni Anthony Matogoro, Kiungo wa chini anaekaba toka mwanzo wa mchezo hadi mwisho, ni
mpiganaji halisi ambae kila timu inatamani iwe na mchezaji wa aina yake. Ni
mrefu na hilo linamsaidia kucheza mipira yote ya juu inayokuja upande wake, ana nguvu pia
ana akili kubwa ya kusoma njia za mpira, hivyo anakua na uwezo mzuri wa kukisia
uelekeo wa mpira, na kufanya iwe rahisi kukutana nao na kuunasa au kuharibu
pale inapobidi.
![]() |
| ANTHONY MATOGORO (KULIA) AKIWA NA KOCHA MSAIDIZI WA MBEYA CITY MAKA MWALWISI |
Siku walipocheza na Azam jijini Dar,
alimpa wakati mgumu mno Humphrey Mieno,
kwani alikua akivuruga kila mpango uliokua ukitaka kutengenezwa, na hata
walipocheza na Simba Dar , alicheza wa kiwango cha juu sana kiasi kipindi cha pili
chote Amri Kiemba alipotea na hakua na madhara yoyote. Katika mchezo na Yanga Dar, alitembea muda wote wa mchezo na Haruna Niyonzima, na kumfanya kila mara awe anagombana na mwamuzi.
Ana uwezo wa kucheza namba zote za
nyuma, pia ana akili sana ya kugawa mipira hata katika nafasi ndogo, hivyo muda
mwingi wa mchezo hua anafanya maamuzi ambayo ni sahihi na magumu kwa mtu
anaekabana nae.
| ANTHONY MATOGORO(no16) AKIWA NA KIKOSI CHA MBEYA CITY |
Anthony Matogoro alizaliwa Mwanza na
kusoma huko huko Mwanza na alianza kucheza soka akiwa na marafiki zake katika timu ya mtaani ya Kambarage iliyopo Mwanza, baadae
viongozi wa timu ya Pamba wakamuona na kuvutiwa na kipaji chake hivyo wakamchukua, akachezea
timu hiyo katika ligi daraja la kwanza na mwaka 2011 kocha wa Mbeya City Juma
Mwambusi akamchukua na kua ni miongoni mwa wachezaji walioipandisha hadi ligi
kuu.
![]() |
| MATOGORO AKIWA MAZOEZINI |
Akiongelea timu yake ya Mbeya City, anasema
ana furaha kucheza katika timu hiyo
kwani ni kama timu ya familia moja, na kocha wao Juma Mwambusi ni sawa sawa na
mzazi wao “Tunafurahia sana kucheza
chini ya kocha Mwambusi, kwani anatufanya kama ni familia moja na kutupa hamasa
wachezaji wote kiasi hata yule ambae hajapangwa anajiona kama vile nae yumo
ndani anacheza, anajituma katika kutufundisha na hata ukikosea ni mwepesi wa
kukukumbusha wajibu wako” alisema Matogoro.
“ Pia kitu kingine kikubwa kinachotufanya
tufanikiwe ni sapoti kubwa na mshikamano wa mashabiki wetu, hua tunajisikia
tuna amani kwa hamasa inayoletwa na mashabiki kila mahali tulipokwenda kucheza,
sidhani kama itakuja tokea mashabiki wakaipenda timu yao hapa Tanzania kama ilivyo kwa hawa
wa Mbeya City, tunawashukuru sana na tuko nao kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo yetu yote iliyo mbele yetu” alimalizia.



No comments:
Post a Comment