Tz prisons kamili kuwavaa azam
Kikosi cha Tz Prisons kipo tayari
kupambana na timu ya Azam wikiendi hii katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara. Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Azam Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar.
Tz Prisons toka mzunguko wa pili uanze
imeonyesha dhamira ya kufanya kweli, kwani katika michezo minne iliyocheza imeshinda
mitatu na kutoka sare mmoja, na mchezo wa mwisho waliweza kuwafunga Ruvu Stars
kwa mabao sita kwa bila hivyo huonyesha ni kwa jinsi gani walivyo katika moto
muda huu.
Akiongelea kuhusu mchezo huo, kaimu
msemaji wa timu hiyo Junior Matukuta amesema timu yake iko vizuri na wachezaji wana ari kubwa sana kwa mchezo wa
kesho na michezo mingine inayokuja. “Katika mzunguko wa kwanza timu ilikua
ikicheza vizuri sana lakini bahati haikua yetu, utaona mwenyewe kila mchezo
tulikua tukicheza kwa kiwango kikubwa lakini mwisho hatupati matokeo mazuri,
ila kwa sasa hivi tuko sawa na tuna uhakika wa kushinda michezo mingi ijayo”
alisema Matukuta.
“Azam ni moja ya timu nzuri hapa
nchini na sisi pia ni wazuri na tupo katika ligi muda mrefu, hivyo hatuna
wasiwasi na mchezo huo” aliongeza Mtukuta.
Katika michezo yake ya karibuni,
wamefanikiwa kutoka sare na Coastal Union ya bila kufungana, wakaifunga Ruvu
Shooting magoli matatu kwa moja, wakaifunga Mtibwa moja bila na kisha mchezo wa mwisho wameifunga Ruvu Stars kwa magoli sita kwa bila.
Wachezaji wote wapo katika hali nzuri na
hadi sasa hakuna majeruhi yeyote.
MUNGU IBARIKI TZ PRISONS…….

No comments:
Post a Comment