Friday, 14 February 2014

Mbeya city;
Ni sisi na  simba

Timu ya soka ya Mbeya City iko tayari kuikabili timu kongwe ya Simba, katika mchezo unaotegemewa kua mkali na wa kuvutia utakaochezwa jumamosi.

       Akiongea kuhusu  mchezo huo, kocha wa timu ya Mbeya City Juma Mwambusi anasema vijana wake wapo tayari kwa mchezo huo.
    “Nashukuru mungu wachezaji wangu wote wapo salama, hata wale waliokua majeruhi sasa hivi wamepona hivyo kunifanya niwe na wigo mpana wa kuchagua watakaocheza, hata wale waliokua na adhabu za kadi kama Steven Mazanda na Hassan Mwasapili, tayari wamemaliza adhabu zao na hivyo wanategemewa kuanza katika mchezo huo” alisema.
kocha juma mwambusi
        Na kuhusu timu yake mara nyingi kufungwa goli la mapema alisema “tayari nimewajenga kisaikolojia hivyo sasa hiv wanajua hakuna tena kusema tunasomana kimchezo, wanatakiwa wawe makini dakika zote za mchezo, na hilo naamin watakua wamelielewa na watalifanyia kazi”aliongeza.

      Akiongelea mchezo huo beki wa kulia wa Mbeya City  John Kabanda  alisema “ tunaamini kila kitu, kitakwenda sawa, kwani tumefanya matayarisho mazuri ya ki mwili na kiakili hivyo kilichobaki ni kwenda kufanya kazi, tunajiamini tutashinda huo mchezo na kukaa kileleni mwa ligi hiyo”alisema .
yohana morris
       Nae Yohana Morris alisema “ki mpira na  ki akili tupo vizuri sana, tunakwenda kupigana ili tushinde, tulishasahau kuhusu timu kubwa na majina makubwa, tunaenda kupambana vitani na kwa matayrisho tuliyofanya tuna uhakika tutashinda”
      KILA LA KHERI MBEYA CITY…

       

No comments:

Post a Comment