Mbeya city sare na simba
Mbeya City imefanikiwa kutoka sare ya goli
moja kwa moja na timu kongwe na ngumu ya Simba katika mchezo mzuri uliochezwa
katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo huo, city walikua wa
kwanza kupata bao lililopatikana kwa njia ya penati baada ya Wiliam Lucien wa Simba kuushika mpira ndani ya eneo la hatari.
Penati hiyo ilipigwa kiufundi na beki
Deogratius Julius na kumfanya kipa wa Simba Beko asiwe na la kufanya.
![]() |
| KIKOSI CHA SIMBA KIKIINGIA UWANJANI. |
Mbeya City walimchezesha beki wake wa
kushoto Hassan Mwasapili kama mshambuliaji na Hamad Kibopile kama mlinzi wa
kushoto, ambae alicheza vizuri sana hadi
alipopewa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Singano hivyo ikambidi kocha wa
Mbeya City Juma Mwambusi afanye mabadiliko ili kumuepusha na kadi nyekundu na
nafasi yake ikachukuliwa na Mwagane Yeya.
City waliutawala mchezo kipindi cha kwanza na Simba wakautawala
zaidi kipindi cha pili.
![]() |
| KIKOSI CHA MBEYA CITY KIKIINGIA. |
Simba walipata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake
hatari Amis Tambwe mwanzoni mwa kipindi
cha pili baada ya kupata mpira toka kwa Haruna Chanongo.
![]() |
| MASHABIKI WAKILANGULIWA TIKETIA |
Tiketi za mchezo huo zilikwisha mapemasana kiasi umati mkubwa wa watu ulibaki nje baada ya kukosa tiketi na walanguzi waliweza kulangua tiketi hizo hadi kufikia shilingi 15000 na 20000.




No comments:
Post a Comment