Peter mapunda
BUNDUKI YA MBEYA CITY
Imeandikwa na
Abdul Sudi, Mbeya/picha kwa hisani ya www.bayana.blogspot na Peter Mapunda.
Mbeya City ina washambuliaji
wengi, na kila mmoja akipata nafasi
anaitumia. Wengi tunamfahamu Mwegane Yeya, ana magoli matano tayari katika ligi
kuu na matatu kati ya hayo aliwafunga Azam, tunamfahamu Paul Nonga, Jeremiah
John na hata Richard Peter, pia tunawafahamu kina Deus Kaseke, Mohamed Kijuso
na Alex Seth, wote wana uwezo mkubwa sana.
Peter Mapunda alipata nafasi ya kucheza
siku walipopambana na JKT Oljoro,
akafunga na walipotoka pale wakaelekea Tabora kucheza na Rhino huko nako
akafunga kisha wakacheza na Tz Prisons pia akafunga na juzi tena amewafunga Mtibwa, hiyo
ni kudhihirisha kwamba ana uwezo mkubwa sana wa kufunga.
| PETER MAPUNDA AKIMTOKA MBUYU TWITE WA YANGA. |
Alizaliwa Songea na kupata elimu yake huko
huko Songea na alianza kucheza mpira katika timu ya mtaani iliyokua ikijulikana
kama Majengo Sports. Na hapo viongozi wa timu ya Polisi wakamuona na kumchukua
ambapo alishiriki lig daraja la tatu kabla hajachukuliwa na timu kongwe ya Maji
Maji ya huko huko Ruvuma.
Baadae kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi
akamuona na kuvutiwa na kipai chake na kuamua kumchukua, ambappo hadi sasa ni
mmoja wa wafungaji tegemezi wa Mbeya City.
Ana kasi na pia anapiga chenga, ana uwezo wa kupiga miguu yote miwili, na ana uwezo wa kushambulia kutokea katikati
au hata pembeni.Na kikubwa magoli yake anafunga kwa njia tofauti, kwa kichwa au
hata kwa miguu yote miwili, wa kushoto na kulia, hivyo kumfanya aweze kufunga
hata katika mazingira magumu.
| PETER MAPUNDA AKIMSUMBUA NADIR HAROUB. |
Akiongelea siri ya mafanikio ya timu
hiyo, peter anasema “kikubwa ni kwamba kila mchezaji aliye Mbeya City ana uwezo
na anastahili kuwepo hapa, hivyo akipata nafasi hua anaitumia kwa uwezo wake
wote, ndio maana huoni kama kuna tofauti mchezaji mmoja akitoka na kuingia
mwingine, pia mashabiki wetu wanatupa sapoti kubwa sana kila tunapocheza,
wanasafir na sisi na kutufanya tujione kila mchezo kama vile tuko nyumbani,
kiufupi Mbeya haina uwanja wa ugenini, viwanja vyote ni vya nyumbani”
| PETER MAPUNDA AKIWA JUMA ABDUL. |
Pia hakuacha kumuongelea kocha Juma
Mwambusi “ ni kocha tofauti sana kwani anatufanya wachezaji wote tujione kama ni
familia moja, habagui mtu na hana mazengwe kama walivyo makocha wengine wengi
tunaowasikia, ukikosea anakuambia kosa lako na maisha yanaendelea, ki ufupi ni
kocha bora sana hapa nchini”. Alimalizia Peter.

No comments:
Post a Comment