Friday, 21 February 2014

Ni coastal  na mbeya city.

   Mbeya City wana mtihani mwingine leo pale wanapokutana na timu ya Coastal Union ya  Tanga katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania, mchezo huo utafanyika katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Azam Tv.
          Katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Mbeya, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, hivyo kuufanya mchezo huo kutabiriwa kua mgumu muda wote.
     Kikosi cha Mbeya City tayari kipo jijini Tanga na asubuhi ya leo kilimalizia matayarisho yake, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokua beki wa kulia John Kabanda mwenye kadi tatu za njano na kiungo wa pembeni Deus Kaseke ambae hakuambatana na timu hiyo.
        Katika michezo yake mitatu iliyopita, timu ya Coastal Union ilifungwa goli moja na Ruvu Shooting,walitoa sare na Prisons na kuishinda Rhino 1-0. Wakati Mbeya City ilipoteza kwa Yanga 1-0, ikaja kuifunga Mtibwa 2-1 na ya mwisho ikatoa sare na Simba 1-1.

 Mbeya City ikishinda mchezo wa leo itafikisha point 38 wakati Coastal watafikisha point 25. 
   Kikosi cha Mbeya City kwa leo ni;
 1- david Buruan
2-Aziz Sibo
3-Hassan Mwasapili
4-Deo Julius
5-Yusuf Abdallah
6-Anton Matogoro
7-Mwegane Yeya
8-Steven Mazanda
9-Paul Nongwa
10-Jeremiah John
11-Peter Mapunda.

No comments:

Post a Comment