Tz prisons wako vizuri….
Timu ya Tz Prisons imetoka sare
ya kufungana magoli mawili kwa mawili na timu ngumu ya Azam fc katika mchezo wa
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam compex Chamazi.
Hadi mapumziko timu hizo zilikua
hazijafungana. Tz Prisons walitawala sana mchezo huo lakini maamuzi mabovu
yaliyokua yakifanywa na mwamuzi wa kati na wasaidizi wake yalisababisha timu hiyo kunyimwa nafasi nyingi za
kuweza kupata magoli.
![]() |
| PETER MICHAEL WA TZ PRISONS AKIUMILIKI MPIRA |
Tz Prisons walikua wa kwanza kupata goli
lililofungwa na Omega Seme dakika ya 49, baada ya faulo yake aliyopiga shuti
kali kumshinda kipa wa Azam Mwadini na kuandika goli hilo.
Faulo hiyo ilipatikana baada ya beki wa
Azam kumfanyia madhambi kiungo wa Tz Prisons Jimmy Shoji ambae alikua katawala
sana katikati.
Iliwachukua Azam dakika mbili tu
kusawaziha bao hilo, faulo iliyopigwa na Salum abubakar ilipigwa kichwa na
Mieno na mpira ukagonga mwamba kisha wakati mabeki wa Tz Prisons wakitaka
kuokoa ukamfikia Agrey Morris aliyepiga kichwa na kusawazisha goli hilo.
![]() |
| GODFREY PASTORY, LAURIAN MPALILE WAKIWA NA JOHN BOKOWA AZAM |
Kabla Tz Prisons
hawajatulia wakafungwa bao jingine, hilo likifungwa na mshambuliaji hatari wa
Azam Kipre Tchetche, aliyeuwahi mpira mrefu huku walinzi wa Tz Prisons
wakidhani ameotea hivyo kumpa nafasi ya kupiga shuti kali lililompita kipa
Mweta na kujaa wavuni.
Tz Prisons walitulia na kufanya
mashambulizi mengi wakipitia upande wao wa kulia ambap Fred Chudu na beki wa
kulia Salum Kimenya walikua wakifanya safari nyingi upande huo na kuwapa shida
walinzi wa Azam.
![]() |
| GODFREY PASTOR AKITIBIWA BAADA YA KUFANYIWA MADHAMBI NA MCHEZAJI WA AZAM |
Kipre tchetche alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira
kwa makusudi hivyo akapewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
Tz Prisons walisawazisha bao la pili kupitia
kwa mlinzi wake wa kushoto Laurian Mpalile baada ya kazi nzuri iliyofanywa na
Jimy Shoji kuupeleka mpira upnde wakulia na Chudu akapiga krosi iliyokutana na
Mpalile aliyeunganisha na kusawazisha.
| MASHABIKI WA TZ PRISONS WAKISHANGILIA TIMU YAO |
Tz Prisons walicheza vizuri katika
mchezo huu, na viungo wake walielewana sana na kutengeneza nafasi nyingi za kuweza kupata ushindi lakini maamuzi hayakua upande wao.
Washambuliaji wake Peter Michael naFrank
Wiliam walikua walicheza kwa uelewano mkubwa sana.
| NYUMBANI NI NYUMBANI!HATA MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIJIUNGA KUSHAGILIA. |
Baada ya mchezo huo, tz Prisons
imefikisha point 20.



This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeletesaaaafi,nmeipenda mashabik wa MCC kusapot tim ya maskanii
ReplyDeletenimeipenda sana prison wako kimya na wanacheza kwa umakini bila kelele
ReplyDelete