Sunday, 23 February 2014

Tz prisons wako vizuri….

Timu ya Tz Prisons imetoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili na timu ngumu ya Azam fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam compex Chamazi.

       Hadi mapumziko timu hizo zilikua hazijafungana. Tz Prisons walitawala sana mchezo huo lakini maamuzi mabovu yaliyokua yakifanywa na mwamuzi wa kati na wasaidizi wake yalisababisha  timu hiyo kunyimwa nafasi nyingi za kuweza kupata magoli.
PETER MICHAEL  WA TZ PRISONS AKIUMILIKI MPIRA
     Tz Prisons walikua wa kwanza kupata goli lililofungwa na Omega Seme dakika ya 49, baada ya faulo yake aliyopiga shuti kali kumshinda kipa wa Azam Mwadini na kuandika goli hilo.
    Faulo hiyo ilipatikana baada ya beki wa Azam kumfanyia madhambi kiungo wa Tz Prisons Jimmy Shoji ambae alikua katawala sana katikati.
      Iliwachukua Azam dakika mbili tu kusawaziha bao hilo, faulo iliyopigwa na Salum abubakar ilipigwa kichwa na Mieno na mpira ukagonga mwamba kisha wakati mabeki wa Tz Prisons wakitaka kuokoa ukamfikia Agrey Morris aliyepiga kichwa na kusawazisha goli hilo.
GODFREY PASTORY, LAURIAN MPALILE WAKIWA NA JOHN BOKOWA AZAM 
         Kabla Tz Prisons hawajatulia wakafungwa bao jingine, hilo likifungwa na mshambuliaji hatari wa Azam Kipre Tchetche, aliyeuwahi mpira mrefu huku walinzi wa Tz Prisons wakidhani ameotea hivyo kumpa nafasi ya kupiga shuti kali lililompita kipa Mweta na kujaa wavuni.
       Tz Prisons walitulia na kufanya mashambulizi mengi wakipitia upande wao wa kulia ambap Fred Chudu na beki wa kulia Salum Kimenya walikua wakifanya safari nyingi upande huo na kuwapa shida walinzi wa Azam.
GODFREY PASTOR AKITIBIWA BAADA YA KUFANYIWA MADHAMBI NA MCHEZAJI WA AZAM
          Kipre tchetche alitolewa  nje kwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira kwa makusudi hivyo akapewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
       Tz Prisons walisawazisha bao la pili kupitia kwa mlinzi wake wa kushoto Laurian Mpalile baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jimy Shoji kuupeleka mpira upnde wakulia na Chudu akapiga krosi iliyokutana na Mpalile aliyeunganisha na kusawazisha.
MASHABIKI WA TZ PRISONS WAKISHANGILIA TIMU YAO
       Tz Prisons walicheza vizuri  katika mchezo huu, na viungo wake walielewana sana na kutengeneza nafasi nyingi za kuweza kupata ushindi lakini maamuzi hayakua upande wao.
  Washambuliaji wake Peter Michael naFrank Wiliam walikua walicheza kwa uelewano mkubwa sana.
NYUMBANI NI NYUMBANI!HATA MASHABIKI WA MBEYA  CITY WALIJIUNGA KUSHAGILIA.

        Baada ya mchezo huo, tz Prisons imefikisha point 20.

3 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. saaaafi,nmeipenda mashabik wa MCC kusapot tim ya maskanii

    ReplyDelete
  3. nimeipenda sana prison wako kimya na wanacheza kwa umakini bila kelele

    ReplyDelete