WATAALAMWA KUPUNGUZA NA KUJENGA MWILI
GOLD GYM MBEYA
Ni kazi rahisi sana kunenepa na
kuharibu shepu yako, lakini ni vigumu mno kuondoa huo unene. Watu wengi
wanatumia gharama kubwa ili kujaribu kupunguza mwili ulioongezeka bila ya
kupenda.
Fikiria, unaamka asubuhi,unakula kisha
unapanda gari na kwenda kazini, ukifika unakaa mezani, unaletewa chai au wengine hata supu, unakula unafanya kazi
kisha mchana unaenda lunch, na baadae jioni unapanda gari unarudi nyumbani.
Unakua hujaushughulisha mwili kwa lolote, bila ya kujijua unaongeza mwili wako
na hadi uje kustuka unakua tayari umechelewa.
UNAKUA huwezi kuvaa nguo za
kukupendeza kwani tumbo litaonekana ni kubwa, unakua unaogopa hata kujitazama
katika kioo kwani unaona wewe sio yule wa zamani uliyemzoea.
Kuna wanaojaribu kufanya mazoezi ili
wapungue, kuna wale wanaopunguza kula (diet) lakini inakua ni ngumu sana
kufikia malengo, na kuna wale ambao kila siku anatoa ahadi kwamba kesho ataanza
mazoezi ili apungue au kesho ataanza kujinyima kula ili apungue, lakini inakua
ngumu, kesho inakua kesho na kesho yenyewe haifiki na mwili unazidi kuongezeka.
Yusuf Chiba anamiliki sehemu ya
kufanyia mazoezi katika eneo la uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,inayoitwa GOLD GYM ana utaalamu wa
muda mrefu kuhusu jinsi ya kuutunza mwili na kuuweka katika shepu unayoitaka.
Anasema kuna njia nyingi sana za kukufanya
upunguze mwili wako “kwanza elewa kitambi au unene unatengenezwa na chakula ambacho umekula na
hakijafanya kazi mwilini, yaani ni chakula ulichozidisha kula, hivyo kinapokua
mwilini hua mara nyingi kinakimbilia au tumboni au katika wowowo, ndio maana
utaona watu wengi wakiridhika na kula vizuri basi lazima ananenepa, pia
unapokula sana vyakula vyenye mafuta ni vigumu sana kusagika hivyo vinazunguka
na kujikuta vimekaa tumbon na kukufanya uwe mnene na kitambi”
“Ili upunguze kitambi au unene inabidi
uyeyushe hayo mafuta na njia ya kuyeyusha kubwa ni kufanya mazoezi, na
inatakiwa ufanye mazoezi kwa kufuata masharti na sio kufanya tu ili uonekane
unafanya mazoezi, kwa mfano, kuna watu
wanafanya sana mazoezi lakini akimaliza anakula chakula kingi na chenye mafuta
na anakunywa juice nyingi yenye sukari ambayo humuongezea
vile alivyopoteza anapofanya mazoezi! Si mara moja au mbili nimeona mtu akitoka
kufanya mazoezi anaenda kupumzika bar na kunywa bia, hivyo inakua haimsaidii
kupunguza mwili bali inamuongeza tu pumzi na kumuweka fit lakini unene unabaki
pale pale” anasema Chiba.
Kwa vile tumekubaliana unene
unasababishwa na chakula ambacho umekula na hakifanyi kazi, nitajaribu kukupa
njia rahisi za kuweza kukusaidia kupunguza unene na kitambi, ni rahisi sana kwa
kuzisoma lakini utekelezaji wake ni mgumu kwa vile inatakiwa nidhamu ya hali ya
juu sana. Lakini kwa vile una nia ya kupunguza
mwili wako hebu jaribu njia hii ;
CHAKULA-
1-Epuka sana kula chakula
chenye mafuta au kinachokaangwa na mafuta, kwani ni vigumu sana kuyeyuka
kinapofika mwilini.
2- kula ili ushibe
tu si kula sana kwa vile chakula kipo.
3-punguza sana
kunywa soda na juice pamoja na bia
4-kua active usikae
sana sehemu moja,jaribu angalau kutembea tembea.
5-fanya mazoezi
kila siku.
NAMNA NZURI YA KUPUNGUZA MWILI
Wengi hua wanajarubu kufanya
mazoezi ya tumbo ili kulipunguza, lakini hilo ni kosa kubwa sana kwani
unapofanya mazoezi ya tumbo unalifanya liwe gumu na lina nguvu lakini kupungua
ni sifuri!!!wengi hawaelewi hilo jambo lakini mazoezi mengi ya tumbo ni
kulifanya liwe strong sio kulipunguza.
Nitakupa njia ya kufanya hayo
mazoezi ukichanganya na diet rahisi ili upungue.
1.
TUKIANZIA katika chakula,
chunguza kwa siku unakula kiasi gani kwa kila mlo, mfano kila asubuhi unakunywa chai
vikombe viwili, chapati mbili, sambusa mbili,juice au soda na glass ya maji.
UNACHOTAKIWA KUFANYA
-kwa wiki ya kwanza
punguza nusu ya unachokula, hivyo asubuhi kunywa chai kikombe kimoja,chapatti
moja,sambusa moja, usinywe juce au soda, kunywa na maji.
-mchana pia punguza
kiasi cha chakula unachokula kiwe nusu ya unachokula kila siku.nadhani mwenyewe
unajua kipimo cha chakula unachokula.
-usiku pia fanya
hivyo hivyo, najua ni vigumu sana lakini nina uhakika na matokeo yake.
MAZOEZI- kwanza hakikisha
umepima una kilo ngapi kabla ya kuanza mazoezi.
-Kila siku fanya mazoezi
mara mbili kwa siku kwa njia ifuatayo
Iwapo hujafanya
mazoezi muda mrefu anza taratibu.
Tafuta kamba ya kuruka na ukiamka tu jambo la
kwanza anza kuruka kamba na njia yake ni kama ifuatavyo.
Wiki ya kwanza ruka mara 30 kisha unapumzika dakika moja,
unaruka tena mara 30 unapumzika dakika moja hadi ufike round 10,kwa maana hiyo
utakua umeruka mara 300. Yaani 30 x10. Kisha ukimaliza kuruka jitahidi upige push
up hata mara 15 kisha kaoge ndio unywe
chai. Na chai inatakiwa unywe kama nilivyoelekeza hapo juu.
Jioni kabla ya kula
rudia tena hayo mazoezi kwa njia ambayo nimekuelekeza , fanya hivyo wiki nzima
na kula kama nilivyoelekeza kwa wiki nzima. Baada ya wiki utakua umeanza kuzoea
hapo unaongeza tena badala ya kuruka mara 30, unaruka mara 50 x 10 iakua ni
mara 500. Na hakikisha unapumzika kwa dakika moja tu usizidishe maana ni muhimu
sana kuufanya mwili usipoe.
MUHIMU- hakikisha unakula saa moja au dakika 45 kabla ya kulala ili chakula ulichokula kifanye kazi, ni mbaya kula kisha unalala,maana hapo chakula kinakua hakijafanya kazi yake na kinageuka kua ni ziada.
WIKI ya tatu punguza
tena chakula kidogo ya kile unachokula, vizuri zaidi kama ukipunguza tena nusu
ya unachokula wakati huo, hivyo ina
maana itakua ni robo ya chakula ulichozoea kula kila siku, Najua ni ngumu mno
kufanya hivyo lakini nakuhakikishia ukija kuzoea utaona ni jambo la kawaida kabisa.
Na hakikisha unaendelea na
mazoezi kila siku bila kufanya uvivu,
utakapojiona unazidi kupata pumzi ongeza lap za kuruka hadi ufike mara
100 au hata 150, ina maana kila chakula ulichokula kitakua kinatumika na pia
utakua unaunguza na mafuta yaliyopo mwilini mwako. Baada ya mwezi nina uhakika
utakua umepungua kwa kiasi kikubwa sana.
Usisahau kupima uzito kila mara ili uone ni kwa kiasi gani unapungua.
KWA WALE WALIOPO JIJNI MBEYA AU
WANAOTAKA KUJUA ZAIDI JINSI YA KUFANYA ILI KPUNGUZA MWILI WAWASILIANE NA YUSUF CHIBA KWA NAMBA YA SIMU 0659 464 344


No comments:
Post a Comment