Kocha mwambusi
BADO TUPO VIZURI
Kocha mkuu wa timu ya Mbeya City,
Juma mwambusi amesema timu yake bado iko vizuri pamoja na matokeo waliyopata
karibuni.
Timu hiyo imetoka sare na JKT Oljoro katika
mchezo wake wa mwisho, na kabla ya hapo ilipoteza kwa timu ya Coastal Union ya
Tanga.
Akiongelea matokeo hayo kocha Mwambusi
amesema “bado nawaamini vijana wangu kwani hadi sasa wako imara na wanajitahidi
kwa nguvu zao kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, kilichotokea ni hali ya
kawaida ya mchezo, hivyo kila ukimaliza mechi moja inatakiwa utazame uliyokosea na
kujaribu kuyarekebisha ili katika mchezo unaofuata usirudie makosa hayo hayo”alisisitiza.
![]() |
| KOCHA MWAMBUSI AKITOA MAELEKEZO(picha toka katika mtandao) |
‘Ukitazama mzunguuko wa kwanza timu
ilionekana iko vizuri sana na kila mtu aliifurahia na kuipa sapoti kubwa, lakini kuna mambo mengi ya kiufundi yametokea
hapo katikati, mfano ligi ilisimama
zaidi ya miezi miwili, na kumbuka wakati huo vijana wangu walikua tayari wako
juu sana ki mchezo na morali pia ilikua iko juu sana, matokeo yake ligi
iliposimama timu nyingine nyingi zilifanya usajili mpya na kurekebisha makosa
yao kwa kujitayarisha upya, na sisi pia tukaanza upya kujitayarisha, lakini
kumbuka morali lazima inakua imeshuka na kuijenga ni kazi kubwa na inayofanyika
taratibu sana, hilo halina ujanja, ndio maana pamoja na mambo mengine madogo
madogo, matokeo yanabadilika”aliongeza kocha.
![]() |
| KOCHA MWAMBUSI |
“Mimi
binafsi natamani kila siku timu yangu ipate ushindi, na ninajitahidi kila siku
kuwafundisha na kurudia kuwafundisha mbinu nyingi na nzuri za kuwafanya wapate
ushindi,ninashukuru wachezaji wangu ni
waelewa mno hivyo tuko pamoja kwa kila kitu, wote tunaumia sana na matokeo haya
lakini ninachofanya kila siku ni kuwaambia mkifungwa sio mwisho wa dunia,
jipangeni ili tuhakikishe tunashinda mchezo unaokuja, wasikate tamaa na kuona
kama vile ndio tumefika mwisho wetu, bado tuna nafasi na tutapigana hadi dakika
a mwisho” alisisitiza.
“Sasa hivi tuna wakati mgumu sana maana tunacheza
na timu ambazo ziko katika hatari ya kushuka daraja, hivyo nazo zinapania sana
zinapocheza na sisi, na pia hata jina letu tulilolijenga nalo linazifaya timu
zipanie kufia uwanjani kila zinapocheza na sisi, hivyo kikubwa ninachofanya ni
kuwaambia vijana wangu, tupambane hadi dakika ya mwisho na INSHA ALLAH
tutashinda mapambano yetu” alimalizia kocha Mwambusi.
Mbeya city mwishoni mwa wiki hii itacheza na timu ya Rhino toka Tabora.


This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete