ATLETICO SARE NA CHELSEA
Atletico Madrid wametoka sare ya bila kufungana na Chelsea katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali wa
klabu bingwa ya Ulaya katika uwanja wa Estadio Vicente Calderon.
Matokeo hayo yamewafanya Chelsea angalau kua na matumaini ya kupita kwa
vile mchezo ujao watacheza katika uwanja wa nyumbani.
Kocha
wa Chelsea atakua na wakati mgumu wa kupanga kikosi chake kwani kipa wa timu
hiyo Petr Cech aliumia baada ya
kugongana na mchezaji wa Atletico katika kipindi cha kwanza, na baadae kipindi
cha pili kapteni wa timu hiyo John Terry nae alitolewa baada ya kuumizwa na mchezaji
mwenzake David Luiz.
Ingawa Chelsea watakua na faida ya kucheza mchezo wa pili nyumbani,
lakini Atletico Madrid wana rekodi nzuri ya kushinda ugenini, kwani
walikwishawafunga Ac Milan, na Porto ugenini kisha waliweza kutoka sare na timu
ngumu na nzuri ya Barcelona ugenini.
Nae
kocha wa Atletico Diego Simeone alisema kila timu imejaribu kucheza kwa ubora
ilioona unafaa, ingawa Chelsea walilinda sana lango lao, hilo
tulilitegemeakwani kwa vile wanacheza ugenini waliona silaha kubwa ni kulinda.
Matokeo haya yanaufanya mchezo kua wazi kwni kwa vile wao kwao lazima wafunge
itatakiwa watushambulie na sisi hao ndipo tutapata nafasi ya kucheza mchezo
wetu tuliozoea.
Chelsea ambao wapo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya
Uingereza, pointi tano nyuma ya wanaoongoza Liverpool,wana nafasi ya kupunguza
hizo pointi, kwani jumapili watakutana.
Frank Lampard alipona kupata kadi baada ya kuugonga kwa makusudi mpira uliokua umepigwa na mchezaji wa Atletico.
Mourinho alisema na michezo miwili migumu, wa Liverpool jumapilia na
baadae jumatano wa Atletico, hivyo anatamani achezeshe wachezaji ambao
hatawatumia jumatano siku anacheza na Liverpool.
Katika mchezo huo, Atletico walitawala sehemu kubwa sana ya mchezo,
lakini mabeki na viungo wa Chelsea walikaba vizuri sana na kufanikiwa kuokoa hatari zote
zilizoelekezwa katika lango lao.

No comments:
Post a Comment