Real yaifunga bayern
Real Madrid imefanikiwa kuwafunga Bayern Munich
1-0, katika ligi ya mabingwa Ulaya mchezo ambao Bayern waliutawala kwa muda
wote.
Goli pekee katika mchezo huo lilipatikana
kipindi cha kwanza likiwekwa wavuni na Karim Benzema katika dakika ya 19 baada
ya kupata pasi toka kwa Coenrao.
Ingawa Bayern waliumilii sana mchezo, lakini Real ndi waliopoteza
nafasi nyingi za kufunga, kwani mara kadhaa walifika golini kwa mashambulizi ya
kushtukiza lakini wakshindwa kufunga.
Christiano Ronaldo ambae alicheza huku
akitoka kaika majeruhi alipoteza nafasi mbili nzuri za kuweza kuwahakikishia
ushindi.
Gareh Bale aliingia mwishoni mwa kipindi cha
pili akimbadili Ronaldo na akaleta uhai baada ya kupiga krosi kadhaa zilizoshindwa
kumaliziwa na washambuliaji wa Bayern.
Arjen roben alikua akiisumbua safu ya
ulinzi ya Real, lakini mara zote waliweza kujipanga na kuondoa hatari nyingi
alizokua akizileta.




No comments:
Post a Comment