Wednesday, 23 April 2014

MOYES ATIMULIWAUNITED

Manchester United hatimaye wameamua kuvunja mkataba na kocha wao David Moyes. Wamemteua Ryan Giggs kua kocha wa muda hadi msimu utakapokwisha.

   Kipigo cha 2-0 toka kwa Everton ndio ilikua msumari wa mwisho kwa Moyes, kwani timu haikucheza vizuri katika kila idara.
siku walipofungwa 1-0 na Liverpool
        Moyes aliteuliwa na Sir Alex Ferguson ili amrithi baada ya kudumu kwa miaka 27 akiwa kocha wa United. Lakini Moyes amedumu kwa miezi kumi tu!.
  Mabingwa hao watetezi wako nafasi ya saba katika ligi, na watamaliza ligi wakiwa na point chache kuliko miaka yote toka ligi kuu ianze.Kipigo cha Everton kilikua ni cha 11 katika ligi msimu huu, na kwa mara ya kwanza toka msimu wa 1995/96 watakosa kushiriki ligi ya mabingwa.
akiwa hajui la kufanya
  Ingawa Moyes mwenyewe  kila mara alikua  akisema anapata sapoti ya uongozi na hata mashabiki, lakini mwisho wa siku wamiliki wameona bora  yaishe .
akilalamika kunyimwa penati na Tottenham
    Wiki iliyopita Moyes alitamka kwamba yupo katika harakati za kufanya usajili makini, na alikua na matumaini ya kusajili nyota kadhaa kabla ya kuanza kwa kombe la dunia, wachezaji kama beki wa kushoto Luke Shaw waSouthamtpton na kiungo wa Sporting Lisbon William Cavalho walikua katika list ya Moyes.
akiwa haamini kipigo toka kwa West Brom

   Baada ya kipigo cha Everton Moyes alisema “kila mmoja anajua sasa hivi tupo katika mabadiliko,kuna mambo ambayo tupo njiani kuyafanya”.
     Wiki iliyopita wamiliki wa timu hiyo familia ya Glazer walimwambia Moyes afanye kila analoweza ili angalau wapate nafasi katika ligi ya Europa. Lakini hilo nalo lilikua shakani baada ya kipigo cha Everton.sasa hivi United wapo point sita nyuma ya Tottenham ambao wako nafasi ya sita na michezo iliyobaki ni minne tu.
shabiki akitaka kwenda kumvamia baada ya matokeo mabovu dhidi ya Man City Old Traford
  Manchester United wamepoteza kwa Liverpool,Manchester City na Everton nyumbani na ugenini, hali iliyosababisha kufikia hata mashabiki kuanza kumlaumu Ferguson kwa kumteua Moyes.
akiwa haelewi kipigo cha city Etihad
    Katika mchezo na Aston Villa, mashabiki waliokua wanampinga Moyes walikodi ndege na kupeperusha bango lililokua likimtaka Moyes aondoke katika timu hiyo.
akijaribu kukimbilia mpira ili aokoe muda dhidi ya Spurs
    Toka aanze kuifundisha United, Moyes alifanikiwa kuifunga timu kubwa moja tu Arsenal, na aliweza kukusanya poini sita tu toka kwa hizo timu kubwa. United pia walipata kiigo cha aibu nyumbani toka kwa West Bromwich na Newcastle na  baadae wakatolewa katika Ligi ya mabingwa na Bayern Munich.Pia walitolewa katika kombe laligi na Sunderland, kisha wakatolewa raundi ya tatu katika kombe la FA na Swansea.
KWA HERI

  




No comments:

Post a Comment