Hamid mohamed
Mbeya city mpya
Mbeya city mpya
Msimu wa ligi kuu ya vodacomTanzania umemalizia,na sasa
hivi mambo yanayojadiliwa ni kuhusu usajili wa timu zitakazoshiriki ligi hiyo msimu ujao. Moja ya
timu hizo ni Mbeya City. Tofauti na timu nyingine, wenyewe wameamua
kuwapandisha vijana wao waliokua timu B ili wakafanye kazi pamoja na kaka zao.
Mmoja wa vijana waliopandishwa
katika timu hiyo ni Hamid Mohamed, anaecheza
kama mshambuliaji wa pembeni. Na pia
hata nafasi za katikati.
![]() |
| Hamid Mohamed |
Alianza kucheza katika timu
ndogo ya magereza Kiwira,kabla hajachukuliwa na timu ya Tz Prisons,
Baadae mwaka jana akajiunga na timu ya Mbeya City B. akashiriki
mashindano ya Mufindi, kisha baadae
mwezi December akashriki katika mashindano ya Uhai Cup. Na muda wote huo
alikua ni kapteni wa timu hiyo ya pili ya Mbeya City.
![]() |
| Hamid akiwa na Yohana Morris |
Baadae mwishoni mwa msimu uliomalizika, kocha Juma Mwambusi akaamua kumpandisha na kua
ni mchezaji wa timu ya kwanza ya timu hiyo.
Na mchezo wake wa kwanza kucheza ligi kuu ni
walipocheza na timu ya Mgambo jijini Mbeya na kuishinda kwa goli moja bila,
alicheza kwa dakika 75 ndipo akabadilishwa na kuingizwa Jeremiah John.
Kwa sasa hivi anaendelea na mazoezi akisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.
Kwa sasa hivi anaendelea na mazoezi akisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu.


No comments:
Post a Comment