Thursday, 17 April 2014

Real yainyoa barca

Real Madrid imeifunga Barcelona na kuweza kuchukua kombe la mfalme, katika mchezo huo Real ilishinda kwa magoli mawili kwa moja.
       Huu unaweza kua ni msimu wa kwanza kwa Barcelona kumaliza msimu bila ya kombe lolote kwani tayari wametolewa katika kombe  la Ulaya na pia wapo katika hati hati ya kupata ubingwa wa La Liga.

          Marid walikuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa na Angel Di Maria baada ya Barcelona kufanya shambulizi na wakapoteza mpira na Luca Modric akampa Bale ambae aliupeleka haraka kwa Isco aliyempa Di Maria na huku Barcelona wakidhani ameotea, aliweza kumchambua kirahisi kipa wa Barcelona Pinto na kuandika bao la kwanza.

            Goli hilo lilizidi kuonyesha kwamba timu ya Barcelona ukuta wake ni dhaifu hasa kutokana na kua majeruhi kwa wachezaji kwa Carlos Puyol na Gerard Pique.
        Barcelona walisawazisha katika dakika ya 68, bao hilo lilifungwa kwa kichwa na Bartra kufuatia kona iliyopigwa na Xavi.

      Goli la pili la aMadrid lilipatikana tena kwa shambulizi la kustukiza baada ya Barcelona kushambulia na walipopoteza mpira na  Bale akaupata nyuma ya katikati ya uwanja, akamzidi mbio beki wa Barca Coentrao, na kisha akamzidi ujanja kipa Pinto na kuupitisha mpira katikati ya miguu ya kipa huyo.
     
    Lilikua ni goli zuri sana lililowafanya Madrid kutwaa kombe la mfalme.
      

No comments:

Post a Comment