NURDIN CHONA
BEKI WA KWELI BONGO
Mshambuliaji aliyeongoza kwa kufunga
magoli katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania, Amisi Tambwe hataki tena kukutana
na beki wa Tz Prisons, Nurdin Chona,
kwani kwa jinsi alivyomzuia, hakua na ujanja wala njia ya kumpita japo mara moja kwa dakika zote tisini walipocheza. Kila alipokwenda
alijikuta Nurdin yupo nae,
akiruka kuufata mpira wanaruka pamoja, ilifikia hadi wakaumia kichwani wote wawili
katika jitihada za kuwania mpira, Nurdin
aliweza kuzuia njia zote kiasi kwamba Tambwe hakupata mipira mingi na hakuweza kabisa kua na madhara. Hali hiyo
pia ilimkuta aliyekua mshambuliaji mrefu wa Yanga Didier Kavumbagu, nae alipewa
shughuli kiasi alipoulizwa baada ya mchezo hakusita kumtaja Nurdin kwamba ni
beki imara na anaijua kazi yake.![]() |
| NURDIN AKIPAMBANA NA SINGANO WASIMBA |
Nurdin mzaliwa wa Kigoma amecheza karibu michezo yote waliyocheza Tz
Prisons, ingawa mwanzoni hawakufanya vizuri lakini mzunguuko wa pili walikua
vizuri sana. “Tulipoanza msimu uliokwisha timu ilikua vizuri, lakini hatukupata
matokeo kutokana na mambo mengi, mojawapo ilikua ni maelekezo ya kocha hayakua
yamekamilika. Lakini baadae alipokuja Kocha Mwamwaja hali ikabadilika, kwani
kwanza alitujenga ki saikolojia kiasi wote tukajiona ni washindani na si
wasindikizaji tena, na akatupa morali ya hali ya juu kiasi tukawa tunajiamini
kwamba kila timu tutakayokutana nayo lazima tutaifunga, na ukweli tulifanikiwa
kwa kiasi kikubwa” alisema Nurdin.
![]() |
| USO KWA USO NA NIYONZIMA |
Alianza kucheza mpira katika timu ya
Nyika fc ya kigoma wakati huo akiwa anasoma na baadae mwaka 2012 akajiunga na
timu ya Tz Prisons ambayo hadi sasa bado anaichezea. Ana nguvu na akili nyingi
awapo uwanjani, hivyo kumpita inatakiwa ujipange na uwe mzuri sana.
“Tz
prisons tuko vizuri na tumejipanga msimu
ujao tushindane toka mwanzo hadi mwisho, yaliyotokea msimu huu hata sisi
yametuumiza, lakini msimu ujao tunajipanga kufanya vizuri michezo yote, kwani
bado tuna kikosi kizuri na wachezaji wenye uwezo mkubwa sana, tazama jinsi Jimy
Shoji anavyoweza kumiliki katikati ya uwanja, naamini ni kiungo bora Tanzania, hata Peter Michael ni
mmoja kati ya wafungaji bora hapa Tanzania, na tuna wachezaji wengi wenye
viwango vizuri na wanajua majukumu yao hivyo msimu ujao Tz Prisons itakua ni
moja ya timu bora katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
![]() |
| AKIMZUIA JERRY TEGETEA |
Nurdin amecheza michezo 22 katika
ligi iliyokwisha, hakucheza michezo minne tu walipocheza na Mgambo, Rhino na
Kagera Sugar zote ugenini, na pia hakucheza siku walipokwaana na JKT Oljoro
nyumbani uwanja wa Sokoine. “ Sasa hivi niko katika mazoezi makali nikijaribu
kutengeneza nguvu ili msimu ujao nipambane
kikamilifu na washambuliaji nitakaokutana nao” alisema Nurdin.
![]() |
| HAPITI MTU |
“ninatamani
sana siku moja nije kucheza soka katika ligi kubwa duniani, hivyo kila mara
najitahidi kuongeza kiwango changu ili siku moja nije kua ni tegemeo la nchi
yangu katika soka, ipo siku naamini haya yatatimia.”alimalizia Nurdin ambae
timu kadhaa zimeanza kumnyemelea ili akachezee katika msimu ujao.





No comments:
Post a Comment