Uhuru selemani
nashukuru nipo
huru
Sio siri, mmoja kati ya wachezaji
wenye vipaji vya hali ya juu hapa Tanzania ni Uhuru Selemani, ambae hadi msimu
wa mwaka 2013/14 unamalizika alikua ni mchezaji wa timu kongwe ya Simba. Lakini
sasa hivi ni mchezaji huru baada ya kukubaliana na timu hiyo kwamba hataweza
kuongeza mkataba.
![]() |
| MAFANIKIO |
Uhuru mwenye uwezo wa kupiga miguu yote na
ni jasiri asieogopa kupita katikati ya mabeki, alisema ameamua kutokuongeza
mkataba ili apumzishe akili yake kutokana na presha ya kucheza katika
mazingira magumu.
“unajua kuna mambo mengi sana yanayofanyika katika hizi timu kubwa, mtu wa
nje haelewi, mchezaji unajitahidi kufanya mazoezi yako binafsi, kisha unafanya na
yale unayoelekezwa na kocha na baadae unajituma zaidi ya uwezo wako ili
kuifanya timu ishinde, lakini kuna watu ambao wanakua karibu na kocha, kwa
ajili ya ubinafsi wao au kwa vile wana malengo yao wanaanza kumjaza kocha
maneno, na kwa vile nae ni binaadamu anaanza kufatilia mabaya unayofanya zaidi
ya kutazama yale mazuri uliyofanya, hivyo matokeo yake unakua unacheza kwa
presha kubwa sana na kushindwa kujua ufanye nini ili kila mtu aridhike”
Kuna muda nilisumbuliwa sana na majeraha, ila kwa sasa hivi sina tena hilo tatizo na ninaomba Mungu anisaidie nisiumie na kupata majeraha makubwa tena, kila mara nilikua nacheza kwa tahadhari kubwa ili nisijiumize tena.
![]() |
| ALIPOKUA MAJERUHI |
Uhuru ambae mwanzoni mwa msimu alikua
akiichezea timu ya Coastal Union kwa mkopo aliendelea “Hakuna asiejua kwamba
ninaipenda sana kazi yangu, ninajitahidi sana kujituma niwapo uwanjani, na
kujichunga nikiwa nje ya uwanja. Kazi yangu ni kucheza soka, na nimekua
najituma sana kuongeza kiwango changu kila siku. Lakini kusema ukweli hadi sasa
hivi sijui Simba wanataka mchezaji wa standard gani ili waridhike na kiwango
chake, kwani mara nyingi unaona kile unachofanya ni bora zaidi ya wanachofanya
hao wanaosifiwa, lakini bado wanakupa lawama na maneno ambayo yanakatisha tamaa
zaidi ya kujenga! hua ninatazama sana kanda za michezo ya Simba kila baada ya
kwisha, ili niangalie kama kuna makosa nirekebishe, lakini hua naona wenzangu
wamefanya makosa mengi zaidi yangu,hawaambiwi kitu, ila mimi nikifanya kosa
moja tu inakua kama ni mimi ndio
niliyesababisha matokeo kua tofauti”
![]() |
| UHURU AKIFANYA MAZOEZI BINAFSI |
“Ninashukuru sasa hivi niko huru, na Mungu
kanisaidia hadi sasa majeraha yaliyokua yakinitesa muda mrefu yamepona hivyo
niko vizuri na ninafanya mazoezi yangu binafsi ili nijipange na maisha mapya
baada ya kumalizana na jinamizi la msimu uliopita, nipo nyumbani Mbeya
ninatarajia Mungu akipenda niende kujaribu kucheza nje ya nchi, kama
itashindikana nitasajili timu nyingine yoyote nifanye kile mabcho ninajiamini
nina uwezo wa kukifanya kwa ubora zaidi.”




No comments:
Post a Comment