Beno kakolanya
TZ PRISONS ONE
Baada ya katikati ya msimu uliopita kuondokewa na aliyekua kipa nambari moja wa Tz Prisons,
Wilbert Mweta, mashabiki wa soka walitegemea timu hiyo itashuka daraja, kwani
katika mzunguuko wa kwanza, ilikua ipo chini kabisa mwa msimamo wa ligi, hivyo
kuondoka tena kwa kipa tegemeo kuliwapa wasiwasi wengi.
Lakini kocha David
Mwamaja aliamua kumuamini kipa mwingine, Beno Kakolanya ashike hatamu za timu
hiyo, na hakumuangusha, kwani alipigana
kiume na kuisaidia timu yake kuondoka katika janga la kushuka daraja. Hata
katika mchezo waliocheza na Ashanti mjini Morogoro, ambao kama wangefungwa
wangeshuka daraja yeye ndie alikua nyota wa mchezo, aliokoa michomo mingi na
hatari nyingi.
![]() |
| BENO KIWA MAZOEZINI |
“Timu yetu ni
nzuri, na tuko vijana wengi ambao tunaelewana, msimu uliopita haukua wetu
lakini ka matayarisho tunayofanya natarajia tutakua vizuri msimu huu tofauti na
uliopita” aliongea Beno “na kocha anatupa mafunzo ambayo tunamuelewa, hivyo
hkuna sababu ya kutoa visingizio tena msimu huu”
Mchezo wao wa kwanza
wanacheza na Ruvu Shooting “ tumejitayarisha kwa michezo yote, tunaanza na Ruvu
kisha tunacheza na Yanga, mechi zote kwetu ni ngumu lakini kwa matayarisho
tunayofanya, tunaamini tutafanya vizuri katika michezo hiyo” aliongeza.
![]() |
| KIKOSI CHA TZ PRISONS |
Beno mzaliwa wa Sumbawanga mkoani Rukwa
anasema anafurahia kuwepo kwake katika timu hiyo ya Tz Prisons “ hapa nina
amani sana kwani wote tunajua malengo yetu, matarajio yangu siku moja na mimi
nipate bahati nionekane na nichaguliwe katika timu ya taifa, kwani ninaamini
uwezo wangu ni mkubwa sawa sawa na hao wanaocheza katika timu hiyo ya taifa”
aliendelea “ nia yangu siku moja niende nje nikaceze mpira wa klipwa, hapo
nitakua na manufaa kwangu mwenyewe na kwa taifa pia, na hilo najua
linawezekana, bado sijafika mwisho wa safari yangu” alisisitiza.
![]() |
| AKIWA ACADEMY YA MBASPO |
Alisoma shule ya
msingi Mwenge Sumbawanga , na sekondari
alianza Kanda huko huko sumbawanga na kumalizia katika sekondari ya Samora
jijini Mbeya. “nilipokua shule nilikua nacheza soka na ndipo nikachukuliwa na
Academy ya Mbaspo na huko nikashiriki
mashindano mengi, nilienda Copa Coca Cola nikiwa nimeonekana katika Academy
hiyo, baadae mwaka jana mwezi wa sita ndio nikahamia Tz Prisons ambayo nipo hadi
sasa,na katika msimu huo nikacheza michezo 18 ya ligi” alisema Beno.
Anasema ligi
msimu huu ni ngumu, lakini anaamini hata timu nyingine zitakuja na tahadhari
pindi wanapochza na Tz Prisons “ tupo vizuri sana na tunategemea kuongezeka
uzuri ligi inavyoendelea” alimalizia Beno.




No comments:
Post a Comment