SIMBA NA
YANGA SASA OCTOBA 18
Shirikisho la
soka Tanzania, TFF limesogeza mbele kwa wiki moja mchezo wa mahasimu wa jadi
Tanzania, Yanga na Simba kwa wiki moja zaidi, na hivyo
sasa utafanyika tarehe 18 octoba badala ya tarrehe 12 kama ilivyokua katika
ratiba ya awali..
Akielezea sababu
zilizofanya kusogezwa mbele kwa mchezo
huo, mkurugenzi wa mashindano wa TFF Boniface Wambura amesema imetokana na
kuingiliana na ratiba ya FIFA ambapo kwa tarehe hiyo timu ya taifa ya Tanzania
itacheza na timu ya Benin.
Kumekua na maoni tofauti kutoka kwa
mashabiki wa timu hizo, wa Yanga wakisema hiyo imetokana na TFF kutaka
kuwasaidia Simba ambao kwa muda mfupi wamepata bahati mbaya ya wachezaji wake
watano muhimu kuumia, hivyo waliogopa iwapo watacheza bila ya hao wachezaji
kuna uwezekano mkubwa kwa tiu hiyo kupoteza mchezo.
Kauli hizo zimepingwa vkali na mashabii wa
Simba, wakiongozwa na mwenyekiti wa usajili wa timu hiyo Zacharia Hanspope
ammbae alisema timu yake iko vizuri idara zote, na kama kuumia kwa hao
wachezaji, wapo wengine wenye kiwango kama hicho ambao wanaaminiwa watafanya
vizuri kama wakipata nafasi, aliongeza kwamba timu yake haiwaogopi Yanga hata
wakiamshwa usiku wa manane wapo tayari kucheza nao na wana uhakika watashinda.

No comments:
Post a Comment