Sunday, 28 September 2014

  Yanga    yawafunga   tz   prisons

     Yanga ilipata goli lake la kungoza la kiufundi llililofungwa na Coutinho katika dakika ya 34, baada ya Mrisho Ngasa kuchezewa vibaya ndipo mwamuzi akatoa adhabu hiyo.
      Kama hiyo haitoshi , dakika nne baadae Prisons walipata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake wenye nguvu Jackob Mwakalobo kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa mchezo mbaya.

 Kipindi ca pili Prisons walibadilika hasa baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Meshack Ernest na umuingiza Julius kwanga na kumtoa pia Amiri Omary na kumuingiza Ibrahim Kahaka ambao walibadilisha kwa kiasi kikkubwa hali ya mchezo huo.
 Tz Prisons walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Ibrahim Kahaka aliyeunganisha kwa kichwa krosi nzuri iliyochongwa na Julius  Kwanga na kuufanya mchezo kua 1-1.
 Lakini  haikuwachukua muda Yanga kupata bao la ushndi kupitia kwa Simon Msuva, bao la aina ile ile kwani nae aliunganisha kwa kichwa krosi ya Mrisho Ngasa, hivyo hadi mwisho Yanga 2 na Tz Prisons 1.

No comments:

Post a Comment