Monday, 22 September 2014

TZ PRISONS YAANZA VEMA
    Timu ya Tz Prisons, ilizima kelele za msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire, baada ya kuwafunga kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo mzuri uliochezwa uwanja wa Mabatini Ruvu.
Tz Prisons ambayo katika mchezo wake wa mwisho wa majaribio kabla ya kuanza kwa ligi, walipoteza kwa idadi kama hiyo ya magoli dhidi ya JKU ya Zanzibar, waliutawala mcheezo kwa kipindi kirefu, na magoli yao yalifungwa na  Laurian Mpalile na Jacob Mwakalobo. Tz Prisons mchezo unaofuata watacheza na timu ya Yanga jijini Dar.
                                    xxxxxxxx
Ndanda FC ya Mtwara,  imeanza vizuri  ligi kuu ya VODACOM baada ya kuwafunga wageni wenzao katika ligi hiyo Standa United kwa jumla ya mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kambarage Shinyanga..
 Ndanda ilipata mabao yake la kwanza likifungwa na Paul Ngalama katika dakika ya 16 ya mchezo. Bao hilo liliwafanya Stand kucheza kwa kutokujiamini na kupoteza mipira mingi bila sababu.
    Katika dakika ya 35 Nassor Kapama aliipatia timu ya Ndanda bao la pili kutokana na mabeki wa Stand kushindwa kuzuia mashambulizi ya Ndanda,  lakini dakika moja baadae Stand wakapata bao lililofungwa na Salum Kamana.
     Dakika tano baadae wakafungwa goli la tatu lililofungwa na Ernest Josef. Kwa ujumla kipindi chote cha kwanza Ndanda waliutawala mchezo huo na kuweza kupata mabao hayo matatu.
      Kipindi cha pili Stand walionekana wamepata uhai na kuweza kuzuia mashambulizi ya Ndanda, lakini dakika ya 90 Ndanda walipata bao la nne na kuufanya mchezo huo kumaliza kwa ushindi wa mabao 4-1.

                          xxxxxxxxxx
Timu ya Yanga, imeanza vibaya ligi ya Vodacom Tanzania baada ya kufngwa magoli mawli na timu ya Mtibwa ya Morogoro. Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro, unawezakusema sababu kubwa iliyofanya Yanga kupoteza mchezo huo ni ubovu wa uwanja huo.
 Mtibwa walipata bao la kuongoza katika dakika ya 16 lililofungwa na Mussa Hassan Mgosi  baada ya kuwahi mpira mrefu uliopigwa na Ame Said na kuubetua ukampita kipa wa Yanga Deo Munishi.
     Yanga walijitahidi kupata bao la kusawazisha lakini ikawa ngumu, kwani  hakukua na ufundi kutokana na ubovu wa uwanja hivyo kuwashinda wachezaji wa Yanga waliozoea kucheza pasi fupi  nyuma na kisha kupiga ndefu kuwapelekea wachezaji wao wa pembeni. Mpira muda mwingi ulikua ukibutuliwa tu na hauna ladha.
    Kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata penati  dakika za mwanzo tu lakini mshambuliaji wake hatari Toka Brazil Jaja alishindwa kufunga baada ya kipa wa Mtibwa  kkuokoa kwa mguu.
    Katika dakika za mwisho za mchezo huo Ame Said aliyecheza vizuri katika mchezo huo aliipatia Mtibwa bao la pili baada ya kkupokea pasi ndefu na kumuhadaa beki wa Yanga Nadir kisha akapiga kiufundi mpira uliomshinda kipa wa Yanga. Hadi mwisho Mtibwa 2 na Yanga hawakupata kitu. 
         Mabingwa watetezi Azam Fc  imeanza vizuri lig hiyo baada ya kupata ushindi mzuri wa mabao matatu dhidi ya moja la Polisi Moro katika mchezo uliochezwa uwanja wa Azam Chamazi.
Magoli ya timu hiyo mawili yalifungwa na mshambuliaji mpya wa timu hiyo Didier Kavumbagu aliyefunga moja kila kipindi na moja likafumgwa na Agrey Morris.

                                               xxxxxxxx
MATOKEO KAMILI YA MZUNGUUKO WA KWANZA NI
MBEYA CITY 0 JKT RUVU 0
STAND UNITED 1 NDANDA FC 4
RUVU SHOOTING 0 TZ PRISONS 2
MGAMBO  2 KAGERA 1
AZAM FC 3 POLISI MORO 1
SIMBA 2 COASTAL UNION 2
MTIBWA 2 YANGA 0

No comments:

Post a Comment